Friday, May 16, 2014

MZEE ANUSURIKA KUTAPELIWA KWA KUUZIWA DHAHABU BANDIA MJINI KAHAMA,MATAPELI WAKUTWA PIA NA NOTI BANDIA ZA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA


Huyu ni mzee Robert Magere aliyetaka kutapeliwa

Watuhumiwa hao wakiwa wamekalishwa chini na Polisi mara baada ya kukamatwa


Haya ndio madini feki waliyokutwa nayo watuhumiwa Jackson Benard Mushobozi(60) na Mikidadi Hasimi(64) wote wakazi wa Bukoba wamekamatwa wakitaka kuuza dhahabu bandia mjini Kahama. 


Hii ndio gari inayotumiwa na watuhumiwa




Jeshi la polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limewashikilia watu wanne kwa tuhuma za kufanya biashara haramu ya kuuza madini bandia.

Sakata hilo limetokea jana Asubuhi katika eneo la benki ya CRDB mjini Kahama ambapo watuhumiwa Jackson Benard Mushobozi(60) na Mikidadi Hasimi(64) wote wakazi wa Bukoba wamekamatwa wakitaka kuuza dhahabu bandia.

Wengine ni Mtoni Jikalu(42) na Mwita Martini(34) ambao nia wakazi wa jijini Mwanza, kwa pamoja walinasa kwenye mtego ulioandaliwa na Robert Magere waliyetaka kumtapeli ambaye aliamua kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wilayani Kahama.


Magere amesema watu hao wanahisiwa kuwa ni matapeli walitaka kumwuuzia dhahabu bandia yenye thamani ya shilingi 4000,000, na wakati anaongozana nao kwenda CRDB benki kuwalipa, alikuwa amekwishawasiliana na Jeshi la polisi wakakamatwa.

Mwandishi wa habari hizi amefuatilia na tukio hilo na kujionea wakati Watuhumiwa wakipekuliwa katika kituo kikuucha polisi mjini Kahama huku wakikutwa na kile kilichodaiwa madini bandia na pesa bandia za ndani na nje ya nchi.

Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara mjini kahama na watuhumiwa kufanikiwa kutoroka kabla ya kutiwa mbaroni.

0 Responses to “MZEE ANUSURIKA KUTAPELIWA KWA KUUZIWA DHAHABU BANDIA MJINI KAHAMA,MATAPELI WAKUTWA PIA NA NOTI BANDIA ZA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA”

Post a Comment

More to Read