Friday, May 16, 2014

MILIPUKO MIWILI YATOKEA,GIKOMBA,NAIROBI.





Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba milipuko miwili imetokea karibu na Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi.


Milipuko ya leo imetokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.

0 Responses to “MILIPUKO MIWILI YATOKEA,GIKOMBA,NAIROBI.”

Post a Comment

More to Read