Friday, May 16, 2014

WANANCHI MBEYA WAONDOLEWA HOFU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE.


Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariamu Mtunguja akitoa taarifa ya ugonjwa wa Dengue kwa waandishi wa habari



SERIKALI Mkoani Mbeya, imewataka  wakazi wa  Mkoa wa Mbeya kuondoa hofu juu ya ugonjwa ulioibuka  nchini wa  Dengue  kwa kuwa mpaka sasa idara ya afya haijapokea kesi ya mtu aliyepatwa na ugonjwa huo.


Akizungumzia hilo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, alisema hadi sasa hakuna mtu au mgonjwa aliyeripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Mtunguja, alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuzagaa kwa uvumi kutoka kwa baadhi ya wananchi ya kwamba ugonjwa huo tayari umebisha hodi Mbeya na tayari kunamgonjwa amelazwa.

Amesema taarifa zilizoenea mtaani zinajengwa na hofu tu na kwamba timu ya wataalamu wa afya imeendelea kufanya kazi muda wote ili kuona kama kuna taarifa za kuwepo au kutokea kwa mtu yeyote mwenye dalili au ugonjwa huo.

Amesema tayari madaktari wa wilaya zote mkoani hapa wamepewa waraka  unaotoa muongozo wa namna wa kushughulikia kwa haraka taarifa zote zinazotolewa na wananchi juu ya mtu yeyote anayeonesha dalili za kuwa na ugonjwa wa Dengue.

Mbali na madaktari, lakini pia ofisi hiyo ya Mkuu wa mkoa imetoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zote suala la usafi.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi kutoka hospitali ya mkoa wa Mbeya, Dk. Grolia Mbwile, alisema licha Tanzania kukumbwa na ugonjwa huo ambao hata hivyo hauna tiba wa kinga, lakini pia umewahi kuibuka katika nchi ya Misri barani Afrika , pamoja na nchi kadhaa katika bara la Asia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na mtafiti wa tabia za mbu kutoka Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI), Dk . Nicholaus Govela alisema ugonjwa wa Dengue unaambukizwa na  mbu aitwae Aedes Egypti.

0 Responses to “WANANCHI MBEYA WAONDOLEWA HOFU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE.”

Post a Comment

More to Read