Friday, May 16, 2014
NOOIJ ATAMBA KUIVURUMISHA ZIMBABWE, MDAU AMWAGA MKWANJA WA MILIONI 5 KAMA TAIFA STARS ITASHINDA.
Do you like this story?
Kocha wa Taifa Stars, Mart
Nooij amesema wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya mechi ya Kombe la Afrika
dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo (Mei 16 mwaka huu), Nooij amesema kabla ya kuja
Tanzania alikuwa akifuatilia Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo anawafahamu
wachezaji wengi.
Amesema wachezaji wanaounda
kikosi chake ni wenye uzoefu na mechi za kimataifa, hivyo wapo tayari kwa ajili
ya mechi hiyo, kwani wamepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye
kambi iliyokuwa Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.
Nooij amesema ujio wa
washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) kutaongeza morali ya kikosi chake.
Samata na Ulimwengu
watawasili nchini Jumamosi mchana, saa 7.30 mchana kwa ndege ya Ethiopian
Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo leo (Mei 16 mwaka huu) wanacheza
mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Hilal ya huko.
Wachezaji waliopo kambini
kwa sasa ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Said Moradi, Oscar Joshua, Kelvin
Yondani, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Himid Mao,
Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Simon
Msuva, Mrisho Ngasa, Khamis Mcha, Ramadhan Singano, John Bocco, Elias maguli na
Kelvin Friday.
Wakati huo huo, timu ya
Zimbabwe (Mighty Warriors) inawasili kesho alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa
ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 27. Kesho saa 4 asubuhi
(Mei 17 mwaka huu) Kocha wa timu hiyo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari
katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Tiketi kwa ajili ya mechi
hiyo zinaanza kuuzwa kesho (Mei 17 mwaka huu) kwenye vituo vya Shule ya
Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora,
OilCom Ubungo, Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala.
Viingilio ni sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 tu.
…MDAU
AAHIDI WACHEZAJI MIL 5/-
Mdau mmoja wa mpira wa
miguu ambaye hataki jina lake litajwe ameahidi kutoa sh. milioni tano kwa
wachezaji wa Taifa Stars iwapo wataifunga Zimbabwe katika mechi ya Jumapili.
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linamshukuru mdau huyo, na linatoa mwito kwa wadau wengine
wajitokeze kutoa motisha kwa Taifa Stars.
Bonasi ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa wachezaji wa Taifa Stars itatolewa kwa mujibu
wa taratibu zilizopo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NOOIJ ATAMBA KUIVURUMISHA ZIMBABWE, MDAU AMWAGA MKWANJA WA MILIONI 5 KAMA TAIFA STARS ITASHINDA.”
Post a Comment