Friday, May 16, 2014
MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZIA MAISHA YA MWALIMU,AUNGANA NA VIJANA WAZALENDO.
Do you like this story?
Vijana wazalendo na wapenda Amani
ambao wamemtembea Mama Maria wakiongozwa na Kiongozi wao anayejulikana kwa Jina
la Mohamed Nyundo, wamesema wako pamoja na familia hiyo na kwamba
wamesikitishwa na kampeni inayoendelea ya kumchafua Baba wa Taifa, kumkebehi na
kumtuhumu kwa Uzushi na uzandiki.
UJUMBE WA VIJANA KULAANI VITENDO
VIOVU VYA KUMVUNJIA HESHIMA BABA WA TAIFA.
Kumekuwepo na kampeni yenye nia
ovu iliyoasisiwa hivi karibuni ya kuharibu taswira na heshima ya Baba wa Taifa
Mwalimu Kambarage Nyerere katika jamii ya kitanzania na kimataifa.
Kampeni hiyo
inayoendeshwa na vibaraka wa nchi za magharibi na Ulaya, wazandiki na maadui wa
Amani ya Tanzania imeendelea kusambazwa kwa kasi na kwa gharama kubwa.
Kutokana na kuwepo kwa Kampeni
hiyo, jumuiko la Vijana Wazalendo na wapenda Amani tumeamua kutoa tamko
hili la kulaani na kupinga vitendo viovu vya baadhi ya watu kumtuhumu,
kumkebehi na kumtukana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa kutambua Mchango wa Baba wa
Taifa kama muasisi wa Taifa hili, mpigania Uhuru shupavu, Shujaa aliyekuwa na
mapenzi ya dhati kwa watu wake na kwa kutambua umahiri na jitihada za kujenga
Taifa lenye Muungano, Umoja, Amani na Utulivu, jumuiko la Vijana wazalendo
limeamua kuukumbusha Umma wa watanzania juu ya mchango wa utumishi uliotukuka
wa Mwalimu Nyerere katika ustawi wa Taifa letu, lakini pia kuhamasisha
watanzania hasa Vijana kuenzi kwa Vitendo moyo wa kujituma,weledi na busara za
kiuongozi, pamoja na ushujaa na ushupavu wa Mwalimu Nyerere.
Sisi Jumuiko la Vijana wazalendo,
tumeona ni vyema kuja kumfariji Mama yetu, Mama Maria Nyerere pamoja na familia
nzima ya Mwalimu Nyerere na Kwamba sisi kama wananchi na Vijana makini
tutaendelea kuwa pamoja na familia katika kupinga na kulaani vitendo hivyo
viovu vya kejeli, matusi, tuhuma na kebehi zinazoelekezwa kwa Baba wa Taifa,
marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa masikitiko makubwa,
tumeshitushwa na kufadhaika kuona chombo kikubwa na taasisi muhimu ambayo ni
muhimili mkubwa wa Serikali kama Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania
linakuwa ndio uwanja wa matusi ya kumtukana muasisi wa Taifa hili,
imetusikitisha na kutufedhehesha. Imefika wakati sasa, kwa Bunge Tukufu la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kudhibiti na kuondoa kinga yake kwa wale wote
ambao kwa ujinga na kutumika wameamua kuanzisha na kuendesha kampeni kabambe ya
kutia doa taswira na heshima ya Baba wa Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZIA MAISHA YA MWALIMU,AUNGANA NA VIJANA WAZALENDO.”
Post a Comment