Sunday, May 18, 2014
TUHUMA NZITO BAJETI NISHATI NISHATI NA MADINI.
Do you like this story?
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mbunge wa Musoma Vijijini,
Nimrod Mkono wameingia katika mvutano baada ya ujumbe wa maandishi wa kutaka
kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kusambazwa kwa wabunge.
Habari
za uhakika zilizopatikana jana zilieleza kuwa kiini cha mgogoro huo ni ujumbe
mfupi (SMS) ambao unamtuhumu Mkono kula njama za kutaka kukwamisha bajeti ya
Wizara ya Nishati na Madini.
Ujumbe
huo unasomeka ”Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri, Sisi wabunge waadilifu tunakiri
kwamba Mhe Mkono ametufuata na kutupatia fedha kila mmoja milioni 3 ili
tukwamishe bajeti ya Nishati na Madini.
Mkono
ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini, alipoulizwa jana kama ni kweli
amelalamika kwa Spika juu ya jambo hilo, alikiri na kusema alichofanya ni
kulalamika kwa Spika na amemwachia alishughulikie.
“Ni
kweli nimelalamika kwa Spika. Unajua taratibu za Bunge ni kuna any complaint
(lalamiko) unaliwasilisha officially (rasmi) kwa Spika… hilo jambo lipo
nimelifikisha kwa Spika wao ndiyo watafuatilia kwa taratibu zao,”amesema.
Alipotafutwa
kwa njia ya simu ili alitolee ufafanuzi suala hilo, Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo alituma ujumbe kwa simu ukisema:
“Tutavuka
tukiwa na ushindi wa maskini na wanyonge wa nchini mwetu. Tutaendelea kujenga
uchumi imara utakaotoa ajira mpya na matumaini mapya kwa vijana, maskini na
wanyonge wa nchini mwetu. Watanzania wamechoshwa na wizi, udalali, ubabaishaji
na rushwa.”
Mkurugenzi
wa shughuli za Bunge, John Joel alipotafutwa jana alisema yeye hana taarifa juu
ya jambo hilo akisema kama lipo, basi huenda likawa mikononi mwa Spika
mwenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TUHUMA NZITO BAJETI NISHATI NISHATI NA MADINI.”
Post a Comment