Friday, June 27, 2014
KOCHA MPYA WA YANGA MARCIO MAXIMO AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI
Do you like this story?
Aliyekuwa
kocha wa Timu ya Taifa ya hapa nchini Maxio Maximo kutoka Brazil amepata fursa
ya kurudi tena hapa nchini, kuja kuisuka vyema timu ya Yanga ili iweze kucheza
katika michuano ya kimataifa.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani, wakala
aliyemleta Maximo, Ally Mlee alisema kuwa, ilimchukua miaka 3 kumuomba kuja
hapa nchini kusuka timu ya yanga, kwa kujali kwake na ukarimu wa watanzania
amekuja tena hapa nchini na amesaini mkataba wa miaka miwili.
Kwa upande
wake Maximo alisema kuwa, amefurahi kuja kusuka timu ya yanga na anamatumaini
itafanya vyema katika michuano mikubwa nje ya nchi lakini hata katika ligi ya
hapa nyumbani.
“Watanzania
ni wakarimu sana ndio maana nimekubali kuja tena hapa nchini kuinoa Yanga,
lakini pia ujio wangu nimekuja na kocha msaidizi ambaye atanisaidia kusimamia
na pia nitapendekeza wachezaji wazuri kutoka katika timu kubwa huko Ulaya, ili
waje kuchezea Yanga lakini pia ni fursa kwa wachezaji wa yanga kujinoa kupitia
wachezaji wakubwa,” alisema Maximo.
Siku ya
Jumatatu timu ya Yanga itaanza mazoezi na mwalimu huyo mpya, maandalizi ya
kujiandaa na ligi mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KOCHA MPYA WA YANGA MARCIO MAXIMO AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI ”
Post a Comment