Friday, June 27, 2014

MADEREVA TAXI MKOANI NJOMBE WAGOMA, KISA USHURU MKUBWA



Madereva na wamiliki wa magari madogo aina ya tax  wamelalamikia kuwepo kwa utaratibu mbovu wa kudai ada za magari pamoja na tozo za ushuru mbalimbali na kuitaka halmashauri kutoa taarifa kwa viongozi wao ili wajue wajibu wao kabla ya kwenda kudai ada na ushuru wa stika za magari.

Wakizungumza madereva na wamiliki hao wakiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Njombe wamesema kuwa wanashangazwa kuona wameanza kukamatwa kwa kutolipia ada ya mwaka ili hali hawajarudishiwa majibu ya makubaliano walioafikiana kwenye kikao cha mwaka 2011 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo kuhusiana na mapendekezo ya ada ya magari hayo.

Aidha wamiliki na Madereva hao pamoja na kulalamikia utaratibu uliowekwa na halmashauri hiyo lakini wamekubaliana  kusimamisha zoezi la kulipa ada  hadi viongozi wa halmashauri hiyo wakalijadili kwenye vikao vya ndani huku baadhi ya madereva waliobadilisha stika kwenye magari yao wakitakiwa kwenda kuyasajili upya.

Wakizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo maafisa biashara wa halmashauri ya mji wa Njombe Petter Kalihose na Edward Mdem wamekubali kusimamisha ada hiyo hadi suala hilo likajadiliwe kwenye vikao vya ndani na mkurugnezi  juu ya kuongezewa kwa muda wa kusajili magari mapya yaliobadilishiwa stika za magari pamoja na Ada ya mwaka huku magari ambayo hayakusajiliwa kabisa wakiendelea na zoezi la kuyakamata.

Diwani wa kata ya Njombe Mjini Agry Mtambo  akiwa kwenye mkusanyiko wa madereva na wamiliki hao amewasihi kwenda kuyasajili  magari yalionunuliwa hivi karibuni na kuwekewa stika za gari lililouzwa huku akisema  halmashauri itaweka utaratibu mzuri wa kudai ushuru na ada za magari  na viongozi  wa tax watajulishwa makubaliano ya kikao cha ndani cha halmashauri hiyo.

Kwa upande wao viongozi wa madereva na wamiliki wa tax Njombe mjini Akiwemo katibu wao Richard Chyonya wamesema halmashauri inatakiwa kuwashirikisha kabla haijachukua maamuzi kwani viongozi wapo wa tax wapo kwa lengo la kuwasiliana na uongozi wa halmashauri ili kudai kodi na ushuru mbalimbali na si kama utaratibu ulioanza kutumika.

Na Michael Ngilangwa

0 Responses to “MADEREVA TAXI MKOANI NJOMBE WAGOMA, KISA USHURU MKUBWA ”

Post a Comment

More to Read