Monday, March 27, 2017
POLISI 40 WAKATWAKATWA MAPANGA
Do you like this story?
Wanamgambo
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamewashambulia na kuwaua kwa
kuwakatakata wanajeshi takriban 40 baada ya kuwavizia katika mkoa wa
Kasai, katikati mwa nchi hiyo, maafisa wa serikali wamesema.
Wapiganaji hao kutoka kundi la Kamwina Nsapu walishambulia polisi waliokuwa kwenye msafara.
Maafisa sita wa pilisi waliowasiliana na Tshiluba waliachiliwa huru, rais wa bunge la jimbo la Kasai Francois Kalamba amesema.
Machafuko jimbo la Kasai yalianza Agosti mwaka jana, pale maafisa wa polisi walipomuua kiongozi wa Kamwina Nsapu.
Shambulio la Ijumaa lililenga msafara wa polisi waliokuiwa wakisafiri kati ya Tshikapa na Kananga.
Gavana wa jimbo hilo Alexis Nkande Myopompa amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu mauaji hayo.
Umoja
wa Mataifa unasema watu 400 wameuawa na wengine 200,000 kuachwa bila
makao eneo la Kasai tangu Jean-Pierre Pandi, kiongozi wa Kamwina Nsapu
alipouawa.
Mauaji
yake yalitekelezwa miezi miwili baada ya Kamwina Nsapu mwezi Juni 2016
kuanzisha juhudi za kutaka atambuliwe kama mkuu wa eneo hilo na kutaka
maafisa wa serikali ya taifa kuondoka jimbo hilo.
Umoja wa Mataifa unasema umepata makaburi 10 ya pamoja ambapo waliouawa katika machafuko hayo walizikwa.
Kadhalika, kuna maeneo mengine saba ambapo inadhaniwa kuna makaburi yaliyozikwa watu wengi kwa pamoja.
Wataalamu
wawili wa Umoja wa Mataifa, Mmarekani na raia wa Sweden, walitekwa
nyara eneo hilo wiki mbili zilizopita pamoja na raia wanne wa DR Congo
waliokuwa wakifanya kazi nao.
Kufikia sasa bado hawajulikani walipo.
DR
Congo imekabiliwa na hali ya wasiwasi kisiasa huku Rais Joseph Kabila
akiendelea kukaa madarakani kwa muda zaidi kuliko alivyoruhusiwa
kikatiba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “POLISI 40 WAKATWAKATWA MAPANGA”
Post a Comment