Sunday, March 26, 2017

WANAWAKE WAKUTWA NA MISOKOTO 2,000 YA BANGI




Watu 25 wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wanashikiliwa na polisi kwa kukutwa na misokoto 4,458 ya bangi, kilo 70 za mirungi na lita 70 za pombe haramu aina ya gongo.

Miongoni mwa wanaoshikiliwa ni wanawake wawili waliokutwa na misokoto 2,000 ya bangi waliyokuwa wanaisafirisha na msafirishaji maarufu wa mirungi aliyekutwa porini na kilo 50 za miharadati hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Francis Massawe akizungumza jana na waandishi wa habari alisema watu hao walikamatwa katika mji mdogo wa Mirerani kwa nyakati tofauti.

“Hivi sasa tunaendelea na uchunguzi wa matukio hayo ila baadhi yao tumeshawafikisha mahakamani ili wakajibu mashataka yao na zoezi la kuwakamata litakuwa ni endelevu,” alisema kamanda Massawe.

Hata hivyo mkazi wa mji huo, Haji Ngokwe alitoa pongezi kwa operesheni za Polisi na kusema kwamba itasaidia kukomesha matumizi yanayofanyika hadharani.

0 Responses to “WANAWAKE WAKUTWA NA MISOKOTO 2,000 YA BANGI”

Post a Comment

More to Read