Sunday, March 26, 2017

WANYWAJI WASHUKURU VIROBA KUPIGWA MARUFUKU




BAADHI ya vijana waliokuwa wakitumia pombe iliyokuwa katika vifungashio vya Nailoni (Viroba) Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameipongeza Serikali kwa kupiga marufuku kinywaji hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwandishi wa Gazeti hili baadhi wa Wananchi wa Mjini Kahama walisema kuwa kitendo hicho kimewasaidia vijana wengi kubadilika kitabia.

Walisema kuwa kwa sasa vijana wengi wamekuwa wakijali hata familia zao tofauti na hapo awali ambapo kiasi kidogo cha fedha walichokuwa wakipata walikuwa wakitumia kununulia pombe hiyo ambayo ilikuwa ikipatikana kwa gharama ndogo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Zongomela, Machibya Jidulamambasi alisema kwa kitendo cha Serikali kupiga marufuku Viroba kimewakomboa Vijana kwani fedha nyingi walizokuwa wakizitafuta ziliishia katika ununuzi wa kilevi hicho.

Diwani huyo pia aliiomba Serikali baada ya kudhibiti Pombe hiyo pia iangalie upande wa pili la kuzua matumizi ya ugoro ambao kwa sasa umeshamiri mjini Kahama.

0 Responses to “WANYWAJI WASHUKURU VIROBA KUPIGWA MARUFUKU”

Post a Comment

More to Read