Friday, March 24, 2017
SASA HIVI WANAFUNZI KUPIMWA 'TB' KWA LAZIMA
Do you like this story?
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amepiga marufuku shule za binafsi na serikali kupokea wanafunzi bila
kupimwa ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB)
Pia
Waziri Ummy ameagiza watu walio katika makundi hatarishi wakiwemo
wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI na wajawazito wafike vituo vya Afya
kupimwa Kifua Kikuu (TB).
Akitoa
maagizo hayo leo Jijini Arusha kwenye maadhimisho ya siku ya Kifua
Kikuu Duniani, Ummy alisema lengo la kupima makundi hayo muhimu ni
kuzika kuenea kwa ugonjwa huo mapema, kwani mgonjwa mmoja ana uwezo wa
kuambukiza watu 20 kwa mwaka kama hajaanza kutumia dawa kitu ambacho ni
hatari.
"Makundi
hatarishi ambayo lazima wapimwe wale wanaoishi na Virusi vya Ukimwi,
watoto chini ya miaka mkutano, wajawazito, wafungwa, watumiaji madawa ya
kulevya, watu wanaougua saratani na kisukari lazima wapime Kifua Kikuu
kwa lazima," amesema
Alisema
tatizo ni kubwa nchini kwani takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO)
kwa Tanzania kwa mwaka 2015 jumla ya watu 160,000 waliugua Kifua Kikuu
kati ya hao watu 62,180 sawa na asilimia 39 tu ndiyo waligunduliwa na
kupata matibabu.
"Hii
inamaanisha katika kila watu 100,000, watu 306 wanaougua ugonjwa wa
Kifua Kikuu kila mwaka nchini na kati ya hao wanaougua inakadiriwa watu
55,000 wanafariki dunia kila mwaka," amesema
Amesema
Mkoa wa Dar esalaam bado unaongoza kuwa na idadi kubwa yawagonjwa wa
kifua kikuu ambapo waliopo ni asilimia 22, ikifuatiwa na Mwanza, Mbeya,
Morogoro, Shinyanga, Arusha, Mara, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.
"Mikoa hii pamoja na Daresalaam huchangia asilimia 63 ya wagonjwa wote waliogundulika nchini mwaka 2015," amesema
Amesema
kutokana na hilo serikali imeweka mkakati kuongeza vituo vyenye mashine
za kisasa za kupima kifua kikuu kutoka mashine 70 hadi kufika mashine
150 ifikapo Desemba 2017 ambapo mashine hizo kila moja ina uwezo wa
kupima wagonjwa 12 kwa siku na ifikapo Juni 2018 hospitali za Wilaya na
Mikoa zitakuwa na mashine hizo zenye uwezo wa kutoa majibu ndani ya saa
mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)