Friday, March 24, 2017

MAJAMBAZI WATEKA MAGARI MATANAO NA KUPORA FEDHA KIBITI



Watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha wameteka magari matano na kupora Sh920, 000 na simu saba za mkononi katika eneo la Kitembo nje kidogo ya mji wa Kibiti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea juzi saa moja usiku na kwamba abiria walioporwa walikuwa wakisafiri kwenye barabara itokayo Dar es Salaam kwenda Mtwara.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Issa Juma, Nassoro Mohammed, Kassim Omari, Issa Juma na Khalifa Mohammed, wote wakazi wa Dar es Salaam. Wengine waliojeruhiwa ni Badru Uwesu mkazi wa Kisemvule, Mkuranga na Edward Safari, mkazi wa Morogoro.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mchukwi walikopelekwa majeruhi, Dk Japhet Guzuye alisema walikuwa na majeraha shavuni, migongoni na shingoni na walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka.

0 Responses to “MAJAMBAZI WATEKA MAGARI MATANAO NA KUPORA FEDHA KIBITI”

Post a Comment

More to Read