Friday, June 20, 2014
KESI TANO ZA MABILIONI USWISI ZACHUNGUZWA.
Do you like this story?
Tanzania
imeomba msaada kwa taasisi iitwayo International Centre for Asset Recovery –
ICAR (Kituo cha Kimataifa cha Urejeshaji Mali) ya Uswisi kuchunguza kesi tano
zinazohusu watu na taasisi zinazotuhumiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini
humo.
Itakumbukwa
kuwa baada ya kuibuka kwa sakata la mabilioni hayo ya Uswisi, Serikali iliunda
kikosi kazi chini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema
kulifanyia kazi.
Gazeti
hili lilifuatilia suala hilo hadi Uswisi na kubaini kuanza kwa uchunguzi huo,
huku fedha nyingi zikitajwa kwamba zinatokana na vitendo vya rushwa.
Akizungumza
na mwandishi wetu mjini Bern, Uswisi hivi karibuni, Mtafiti wa Sheria wa ICAR,
Andrew Dornbierer alisema: “Tuna makubaliano na Serikali ya Tanzania hasa Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), tunachunguza kwa kina kesi za rushwa na
utoroshwaji wa fedha, hivyo tuko katika ukusanyaji wa taarifa.
Siwezi kukupa
mifano ya moja kwa moja kwa sababu bado tunazifanyia kazi na tunadhibitiwa
katika utoaji wa taarifa.”
Mkurugenzi
wa ICAR, Gretta Fenner Zinkernagel alithibitisha uwepo wa kesi hizo za Tanzania.
“Ni
kweli tumeombwa na Serikali ya Tanzania kusaidia kuchunguza baadhi ya kesi…
zilikuwa zimeshachunguzwa lakini kutokana na uwezo wao mdogo tunawasaidia. Kwa
harakaharaka naweza kusema tunazo kesi tano hivi… ni kesi za watu binafsi na
taasisi na zinahusu masuala ya fedha. Hatuwezi kutaja majina kwa sababu
tunakatazwa kabisa na mkataba wetu na taasisi tunazofanya nazo kazi.”
Licha
ya kutotaja majina, Zinkernagel alisema wanaochunguzwa katika kesi hizo
wanahusishwa na kampuni hewa zilizoanzishwa kwa lengo la kuchota fedha kisha
kwenda kuzificha nje ya nchi.
“Kuna
watu wenye masilahi binafsi na wamekuwa wakipokea rushwa au wamekuwa wakitumia
mashirika kwa ubia au kampuni kivuli na ushirika mwingine wa kimataifa ili
kusafirisha fedha kwenda kwenye kampuni fulani kwa lengo la kuzificha. Ni
kampuni zinazotumiwa na wafanyabiashara kuhamisha fedha haramu na mwisho
hujisafisha,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KESI TANO ZA MABILIONI USWISI ZACHUNGUZWA.”
Post a Comment