Friday, June 20, 2014
TRENI YA MWAKYEMBE YASITISWA KWA MUDA WA SIKU 3
Do you like this story?
. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imesitisha usafiri wa
treni jijini Dar es Salaam kwa siku tatu kutokana na sababu za kiufundi.
Katika
taarifa yake iliyotolewa jana, kaimu mkurugenzi mtendaji wa TRL, Mhandisi Elias
Mshana alisema safari hizo zilisitishwa tangu jana. Amesema uamuzi huo
ulifikiwa ili kufanya ukarabati wa injini za vichwa vya treni .
“Ukarabati
unafanyika katika karakana kuu ya TRL iliyopo Morogoro, tunatarajia vichwa
hivyo vitarejeshwa Dar es Salaam Jumapili,” amesema Mshana.
Amesema
treni itaendelea na ratiba yake kuanzia Jumatatu ijayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRENI YA MWAKYEMBE YASITISWA KWA MUDA WA SIKU 3”
Post a Comment