Friday, June 20, 2014

KUTANA NA MTOTO HUYU MWENYE MKIA ANAYEABUDIWA KAMA MUNGU HUKO INDIA





Mvulana mdogo aliyezaliwa na mkia unaofikia urefu wa inch saba anatarajia kufanyiwa upasuaji ili utolewe licha ya kuwa anaabudiwa kama Mungu na watu wa jamii yake.
Arshid Ali Khan, mwenye miaka 13 anaweza kuathiriwa ukuaji wake kutokana na mkia huo ingawa unamfanya aonekana kama alama ya uponyaji katika Jimbo la Punjab, India. 

Mtoto huyo anayetumia kiti cha watu wenye ulemavu amekuwa akiabudiwa na watu wa jamii yake kama Mungu aliyepewa jina la Balaji.

Khan anasema mkia huo amepewa na Mungu na anaabudiwa kwasababu ni Mungu huyo huyo ndiye anayemuomba ambapo maombi ya watu hugeuka kuwa kweli.

Anasema hajisikii vizuri wala vibaya kuwa na mkia huo yeye anaona sawa tu.
Arshid sasa anaishi na babu yake Iqbal Qureshi, na wajomba zake wawili baada ya baba yake kufariki akiwa na umri wa miaka sita na mama yake kuolewa tena.

0 Responses to “KUTANA NA MTOTO HUYU MWENYE MKIA ANAYEABUDIWA KAMA MUNGU HUKO INDIA”

Post a Comment

More to Read