Wednesday, June 25, 2014

MAPACHA WAIJIBU KAULI YA LULU KUWA HAWAJAMSHIRIKISHA KWENYE WIMBO WAO MPYA, WADAI LULU ANA DHARAU



Baada ya Elizabeth Michael kukana kushirikishwa na kundi la mapacha kwenye wimbo wao mpya ‘Time For The Money’. Kundi la Mapacha limeeleza jinsi lilivyoipokea taarifa hiyo.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Kulwa wa Mapacha amesema kitendo alichokifanya Lulu ni dharau kubwa kwao na kwamba inawezekana ameona hataki kusikika kwenye wimbo waliofanya wao.

“Sisi tuliamua kumtaja kwa respect kwa kuwa tulipenda alichofanya kwenye ile beat ambayo sisi tuliamua kuiimbia kwa kutumia chorus yake. Lakini yeye ameamua kutu-disrespect. Sasa sisi tumeamua hata kama wimbo huo ukipata tuzo basi yeye hatutamtaja...ametudharau.”Alisema Kulwa.
Aliongeza kuwa hivi sasa wameamua kulifuta jina la Lulu na kwamba hata wimbo huo utakapokuwa unapigwa asitajwe kabisa.

“Sasa hivi tunasimama kama Magenge peke yetu. Tumeachana na masuala ya Lulu, hatutamtaja
na tunafuta jina lake kabisa sasa hivi tunabaki Magenge tu.”
Tulipomuuliza kwa nini hawakuwasiliana nae awali angalau kumshukuru kwa chorus aliyowafanyia ili wapate mrejesho mapema. Alisema wao hawajawahi kuonana nae wala kuwasiliana nae hata siku moja.

“Tungewasiliana nae vipi, si unajua hawa watoto unaweza kuwapigia simu wakaacha hata kupokea..si unajua mwanangu. Sisi tungempata wapi sasa. Tud yeye alituambia ni Lulu na sauti yake kweli ni yeye. Sasa kama anakataa bana tunaachana nae."

Baada ya Mapacha kutambulisha wimbo wao na taarifa kumfikia Lulu leo, aliandika kwenye Instagram kwa mshangao mkubwa.

Mwe mwe mwe...!Mbona mnaninyasanyasa...'in Senga's voice'
I swear sina idea na Huku kushirikishwa....au kuna Elizabeth Michael'Lulu' mwingine!????
Dah...hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.”

0 Responses to “MAPACHA WAIJIBU KAULI YA LULU KUWA HAWAJAMSHIRIKISHA KWENYE WIMBO WAO MPYA, WADAI LULU ANA DHARAU ”

Post a Comment

More to Read