Wednesday, June 25, 2014
YANGA WAANZA KUNOA MAKALI COCO BEACH, MAXIMO ATARAJIWA KUWASILI KESHO
Do you like this story?
MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka Tanzania
bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam imeanza mazoezi ya kujiwinda na msimu wa
2014/2015 wa ligi kuu na kombe la Kagame katika Fukwe za Coco Beach jijini Dar
es salaam.
Mazoezi hayo yapo chini ya kocha wa
makipa, Juma Pondamali `Mensah` wakati huu klabu ikimsubiri kocha mpya,
Mbrazil, Marcio Maximo ambaye anatarajia kuwasili kesho kama mambo yatakwenda
kama yalivyangwa.
Mazungumzo ya Maximo na Yanga sc
yalisimamiwa na bosi mwenyewe, Yufus Manji, hivyo kwa asilimia nyingi, Mbrazil
huyo mwenye heshima zaidi nchini Tanzania kutokana na mafanikio aliyoyapata wakati akiifundisha
Taifa stars atatu kukinoa kikosi hicho chenye masikani yake mtaa wa Jangwani
kariokoo jijini Dar es salaam.
Wakati Yanga wakiendelea kumsubiri
Maximo, tayari aliyekuwa kocha msaidizi, Charles Boniface Mkwasa ameshaondoka
na kuelekea Uarabuni.
Mkwasa amepata kazi nchini Saudi Arabia
na taarifa zilibainisha kuwa ameenda kuungana na aliyekuwa bosi wake Yanga,
kocha mholanzi, Hans Van der Pluijm alitetimka kwa makubaliano baada ya mkataba
wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.
Yanga imeweza kuweka wazi majina ya
awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi
kuu.
Msimu uliopita Yanga ilikuwa na kikosi
cha wachezaji 30 kutoka timu ya Wakubwa na wachezaji watano (5) kutoka timu ya
vijana (U20) waliokuwa wamepandishwa kwa ajili kupata uzoefu na
kuiongozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo mbalimbali.
Hata hivyo kutokana na ripoti ya benchi
la ufundi iliyowasilishwa mara baada ya ligi kumalizika, wachezaji 11 wameachwa
katika usajili na tayari uongozi umemalizikana nao na kuwa huru kutafuta timu
nyingine.
Wachezaji hao ni: David Luhende,
Athuman Idd "Chuji", Geroge
Banda -U20, Yusuph Abdul -U20, Rehani Kibingu -U20, Hamisi Thabiti, Reliants Lusajo, Bakari Masoud - U20, Shaban Kondo,
Abdalllah Mguhi "Messi" U-20 na Ibrahim Job .
Yanga
imewaongezea mikataba ya miaka miwili miwili wachezaji wake Jerryson
John Tegete, Said Bahanuzi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ally Mustapha
`Barthez`, Mbuyu Twite, Juma Abdul,
Oscar Joshua, Simon Msuva.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “YANGA WAANZA KUNOA MAKALI COCO BEACH, MAXIMO ATARAJIWA KUWASILI KESHO”
Post a Comment