Wednesday, June 25, 2014
KAMPUNI YA BIDHAA YAMCHANGANYA BARACK OBAMA NA CHRIS SMALLING KATIKA UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA KUHAMASISHA MASHABIKI TIMU YA UINGEREZA.
Do you like this story?
KOMBE
LA DUNIA 2014 NCHINI BRAZIL, Limekuwa
si tu kombe la dunia la kusahau kabisa kuwazungumzia Uingereza dimbani kwa
kusahau kama nao wanashiriki kombe hilo, bali pia limekuwa ni kombe ambalo hata
baadhi ya makampuni yamepata ugumu kuweka picha sahihi za wachezaji wa timu
hiyo ya taifa kwenye bidhaa za promosheni, kwani takwimu zinaonyesha wachezaji
wa timu hiyo ya Uingereza hawajafanya lolote jipya ambalo lingeweza kuwafanya
taswira zao kukaririka na kubakia vichwani mwa watu.
Kampuni
moja lililojikita katika utengenezaji wa thamani za majumbani ambalo
linategemea kuvuna fedha nyingi kwa kuuza vikombe vya kunywea chai na kahawa
vyenye picha za wachezaji wa timu za mataifa mbalimbali yanayo shiriki Kombe la
Dunia ikiwemo timu ya Taifa ya Uingereza, limejikuta kwenye mkumbo huo wa
kutobaini utofauti wa picha ya mchezaji Chris Smalling na ile ya Rais wa
Marekani Barack Obama.
Unaweza
kununua bila utata vikombe vya wachezaji kama Steven Gerrard or Joe
Hart or Wayne Rooney na wengineo lakini utata
unakuja pale utakapo kuwa shabiki wa Chris Smalling na kuhitaji kikombe
cha mchezaji huyo, utakutana na kitu cha utofauti na utastuka ukijiuliza
maswali.. Jeh na huyu tena rais wa nchi nyingine ni mchezaji wa Uingereza?!!
Rais
wa Marekani Barack Obama hachezi kama mtu wa kati kwa klabu ya Manchester United na wala timu ya taifa ya
Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KAMPUNI YA BIDHAA YAMCHANGANYA BARACK OBAMA NA CHRIS SMALLING KATIKA UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA KUHAMASISHA MASHABIKI TIMU YA UINGEREZA.”
Post a Comment