Wednesday, September 14, 2016
MAJAMBAZI YAVAMIA MAGARI YA MNADANI NA KUMUUA DEREVA KWARISASI
Do you like this story?
Majambazi
wapatao 10 juzi usiku walivamia magari mawili yaliyobeba wafanyabiashara
waliokuwa wakitokea mnadani na kumuua kwa risasi, dereva aliyegoma kuwapa fedha
na simu.
Dereva
huyo, Chrispin Inyangwe (40) alipigwa risasi ya mgongoni alipojaribu kupambana
nao.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la katikati ya vijiji vya Miula na
Kalundi vilivyopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema wafanyabiashara hao walikuwa
wakitokea mnadani na walipofika eneo hilo walikuta mawe yamepangwa barabarani
kuzuia magari.
Alisema
baada ya kuona mawe hayo, magari hayo yalilazimika kusimama na ndipo majambazi
hao waliokuwa na silaha za moto, mapanga na marungu walipoibuka na kufyatua
risasi hewani na baadaye kutaka wafanyabiashara hao wasalimishe fedha na simu
zao za mkononi.
Kamanda
huyo alisema baadhi ya wafanyabiashara walisalimisha fedha na simu zao, na
waliokataa walishambuliwa.
Inasemekana
kwamba Inyangwe ambaye alikuwa dereva wa gari aina ya Mitsubishi Canter
alikaidi kutoa fedha na kutaka kupambana nao, ndipo watu hao waliokuwa na
bunduki aina ya SMG walipomfyatulia risasi iliyompata mgongoni na kufariki
dunia papo hapo.
Kitendo
hicho kiliwafanya wafanyabiashara wengine waliokuwa wakikataa kutoa fedha,
kuzisalimisha sambamba na simu zao, ndipo majambazi hao walipowaachia na
kukimbia.
Watu
19 waliojeruhiwa walipelekwa Hospitali ya Mkoa mjini Sumbawanga. Kamanda Kyando
alisema majeruhi 12 waliruhusiwa kurejea nyumbani na wengine saba wanaendelea
na matibabu na kwamba polisi wanaeendelea na msako wa watu hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAJAMBAZI YAVAMIA MAGARI YA MNADANI NA KUMUUA DEREVA KWARISASI ”
Post a Comment