Wednesday, September 14, 2016

MHASIBU WA TAKUKURU ANAYEMILIKI VIWANJA 25, NYUMBA 11 ZIKIWEMO GHOROFA 7 ATIMULIWA KAZI




Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemfukuza kazi Mhasibu wake baada ya kubainika ana utajiri mkubwa wenye utata ikiwamo kumiliki nyumba saba za ghorofa na viwanja 25 hapa nchini.

Uamuzi huo umefuatia kutiwa hatiani na Kamati iliyoundwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo,Valentino Mlowola. Mhasibu huyo amepewa nafasi kukata rufaa katika kamati ya usimamizi ya TAKUKURU. Jina la Mhasibu huo limehifadhiwa kwakuwa hakupatikana kuhojiwa na gazeti la Mwananchi.

Chanzo: Mwananchi,uk. 1&3


0 Responses to “MHASIBU WA TAKUKURU ANAYEMILIKI VIWANJA 25, NYUMBA 11 ZIKIWEMO GHOROFA 7 ATIMULIWA KAZI”

Post a Comment

More to Read