Wednesday, September 14, 2016
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA ZAIDI YA SH BIL. 1.4 KWA AJILI YA MAAFA YA TETEMEKO LA KAGERA
Do you like this story?
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea michango wa zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa
mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa
Kitanzania kwa ajili ya kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi
lililotokea Mkoani Kagera.
Tetemeko
hilo lilitokea Jumamosi, 10 Septemba, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17 hadi
leo na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa
makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo
majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.
Akizungumza
katika hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga hao jana
Jumanne, 13 Septemba, 2016 Waziri Mkuu aliwashukuru kwa michango yao ya fedha
na vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko 2,800 ya saruji. Amesema tetemeko hilo ni
kubwa na halijawahi kutokea nchini.
Alisema
tetemeko hilo limesababisha Serikali kuzifunga shule zake mbili za sekondari za
Nyakato na Ihungo kati ya nne zilizoathirika vibaya na tetemeko hilo.
“Serikali
itajitahidi kuhakikisha inarejesha miundombini iliyoharibiwa na tetemeko hilo
katika kipindi kifupi ili wanafunzi na wananchi wengine waweze kuendelea na
shughuli zao za kawaida,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema katika kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa haraka tayari
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Jenista Muhagama yuko mkoani Kagera akiongoza kitengo cha maafa
kufanya thamnili kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.
Mawaziri
wengine walioko mkoani Kagera wakiendelea kufanya tathmini hiyo ni pamoja na
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
Alisema
Kamati ya Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Maafa ya
mkoa wa Kagera imefungua akaunti maalumu katika benki ya CRDB kwa ajili ya
kupokea michango kutoka kwa watu mbalimbali. Namba za akaunti hiyo ya Kamati ya
Maafa ya Kagera ni CRDB 0152225617300.
Pia
Waziri Mkuu aliwapongeza na kuwashukuru waheshimiwa Wabunge kwa kuamua kutoa
posho zao za kikao cha jana kwa ajili ya kuchangia wahanga wa tetemeko hilo na
kuwaomba wananchi wengine kujitokeza na kutoa michango yao.
Wakati
huo huo viongozi wa makampuni ya mafuta ya GBP, Oil Com na Moil wameahidi
kujenga shule mbili za Nyakato na Ihungo ambazo sehemu kubwa ya miundombinu
yake imeharibika vibaya. Shule hizo zitajengwa katika kipindi cha siku 30.
Hafla
hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu ilihudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara,
Charles Mwijage, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dk. Suzan Kolimba na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi, Dk. Aziz
Mlima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA ZAIDI YA SH BIL. 1.4 KWA AJILI YA MAAFA YA TETEMEKO LA KAGERA ”
Post a Comment