Friday, June 27, 2014
MWANAMKE ALIYEACHIWA HURU NA MAHAKAMA NA KUTEKWA NA KUNDI LA WATU 40 AACHIWA TENA
Do you like this story?
Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo
kwa madai ya kuasi dini ya kiislam ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa
mara ya pili.
Meriam Ibrahimu alikwenda katika
ubalozi wa Marekani uliyopo mji Mkuu wa Khartoum.
Mumewe ana asili ya Sudan Kusini lakini
kwa sasa ni raia wa Marekani.
Mwanamke huyo aliachiliwa baada ya
kuhukumiwa adhabu ya kifo siku ya jumatatu lakini alishikiliwa tena na polisi
kwa tuhuma za kughudhi hati za kusafiria ili aondoke nchini Sudan kwenda
Marekani.
Kufuatia kuachiliwa huru kwa mara
nyingine, Mke huyo wa Ibrahim ameiambia BBC kwamba ataendelea kuwa Mkristo.
Kesi yake ya kuasi dini imevuta hisia
za watu wengi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu pamoja na nchi za
Magharibi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANAMKE ALIYEACHIWA HURU NA MAHAKAMA NA KUTEKWA NA KUNDI LA WATU 40 AACHIWA TENA ”
Post a Comment