Sunday, June 22, 2014
SIRI NZITO BIDHAA ZA MACHINGA.
Do you like this story?
Katika
eneo la mnada wa kuuza vitu vya machinga vilivyokamatwa lililopo katika Soko la
Kibasila Gerezani, kulikuwa na makundi ya watu wa aina mbili; waliokwenda kununua
vitu vingi kwa bei ndogo na wengine ni wale ambao bidhaa zao ndizo zilikuwa
zinapigwa mnada na hawakuwa na uwezo wa kushinikiza wauziwe wao.
Wafanyabiashara
waliokuwapo katika eneo hilo jana, walisikika wakisema wamekwenda kununua vitu
vya dhuluma na kwamba walilazimika kununua kwa kuwa hakukuwa na njia nyingine
ya kufanya.
Leonard
Mwagike alisema baada ya bidhaa zake kukamatwa alijaribu kwenda kuzikomboa
lakini alishindwa baada ya Mahakama ya Jiji kumwamuru alipe faini ya Sh400,000.
“Kinachoendelea
hapa ni dhuluma tu, haiwezekani mzigo wangu wa Sh50,000 uniambie nilipe faini
ya Sh400, 000, bora kuja hapa kuununua tena kama nitaweza,” alisema kwa huzuni.
Mfanyakazi
wa kampuni moja ya udalali jijini, iliyopewa mamlaka ya kuuza bidhaa hizo,
alikuwa akifungua mzigo mmoja baada ya mwingine na kuwataka wafanyabiashara hao
wapange bei.
Hata
hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, alionekana kutaka kuchukua kila bidhaa
aliyoiona ni nzuri, huku akiwaambia wanunuzi kuwa alikwishaichunguza mizigo
hiyo kwa hiyo anajua upi ni mzuri.
Mzigo
wa kwanza kufunguliwa ulikuwa una vyombo vya plastiki vya kuwekea chakula,
ambavyo vyote viliuzwa kwa Sh10, 000. Zilifuata nguo za watoto na chupa za
chai, kisha ukafika wakati ulioleta msuguano kiasi cha kutishia mnada
kuvunjika.
“Sasa
kwenye mzigo huu kuna mali nzuri wengine wameshaiona si ndiyo? Eeh! Ni madera
(magauni), mfuko mzima shilingi ngapi?” Anauliza dalali, lakini kabla hajapata
jibu anasema:
“Jamani
yupo shemeji yenu (mke wake) lazima naye apate hizi nguo (huku minong’ono
ikianza kusikika anachukua magauni matatu na kuyaweka pembeni).”
Kitendo
hicho kiliwakasirisha baadhi ya machinga waliokuwapo katika eneo hilo, huku
wakisema iwapo angeuona mapema mzigo huo angeuchukua wote.
“Mali
mmetunyanganya sisi na hata tunazonunua hapa mtazichukua tena, halafu bado
mnachukua hata mnazouza, hili halikubaliki,” alisema mfanyabiashara mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIRI NZITO BIDHAA ZA MACHINGA.”
Post a Comment