Thursday, July 10, 2014

BOKO HARAM WAZUNGUMZIA HALI ZA WASICHANA ZAIDI YA 200 WALIOWATEKA.



Mmoja wa wanajeshi wa Boko Haram ambaye hakutaka kujitambulisha jina alizungumza na BBC jana (July 8) na kueleza hali na afya ya wasichana zaidi ya 200 wanaoshikiliwa na kundi hilo, taarifa ambazo zilikuwa tofauti na zile za awali zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa Nigeria.

Mtu huyo alisema kuwa wasichana hao wako katika hali salama na wana afya njema tofauti na ripoti alizozitoa Senator kuwa walikuwa wakibakwa wakichukuliwa video na wengine wakiuawa endapo wangekaidi.

Hata hivyo mtu huyo aliweka wazi msimamo wa kundi hilo kuwa watawaachia wasichana hao siku moja baada ya serikali ya Nigeria kuwaachia wafungwa wa kundi hilo wanaowashikilia.

Hivi ndivyo alivyoeleza:
“Kweli tunataka serikali ya Nigeria kuwaachia watu wetu. Kama kiongozi wetu Abubakar Shekau alivyoahidi kwenye vyombo vya habari, kama leo serikali itaawaachia watu wetu, kesho au siku inayofuata tunaahidi mtawaona wasichana wote. Tutaweza kuwaachia kesho ama siku inayofuata. Ninawaambia ukweli, wako katika hali nzuri wakisubiri kuachiliwa. Hawana tatizo. Baadhi wamebadili dini na kuwa waislam, wengine hawakubadili dini lakini hatukuwatofautisha, tunawatunza kwa usawa...”

0 Responses to “ BOKO HARAM WAZUNGUMZIA HALI ZA WASICHANA ZAIDI YA 200 WALIOWATEKA. ”

Post a Comment

More to Read