Friday, July 18, 2014
TRAFIKI 27 WATIMULIWA KAZI KWA KULA RUSHWA.
Do you like this story?
Askari
27 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani wamefukuzwa kazi ndani ya
kipindi cha miezi sita kutokana na kujihusisha na makosa ya rushwa.
Kikosi
hicho ambacho kimeonya dhidi ya unyanyasaji na ushawishi wa rushwa kwa waendesha
pikipiki (bodaboda), kimesema mikakati ya uchunguzi na upelelezi imeimarishwa
kwa lengo la kudhibiti matukio ya rushwa miongoni mwa askari wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani, Taifa, Mohamed Mpinga alisema askari hao wamekamatwa
kutokana na kuimarishwa kwa usimamizi wa nidhamu na mapambano dhidi ya
rushwa.
Alisema,
licha ya kufanya kazi kwa weledi, upo usimamizi wa karibu kwa askari wake
kwa lengo la kuepusha jeshi hilo na matukio ya aibu yakiwemo ya kujihusisha na
rushwa.
"Pamoja
na jitihada hizi tunaomba wananchi wote kutupa ushirikiano kupambana na
hali hii hasa kwa kutoa taarifa za askari wanawaomba rushwa,” alisema Mpinga.
Alisema
taarifa zitawezesha kuwashughulikia kikamilifu askari husika.
Kamanda
Mpinga ameelekeza wananchi hao hususani madereva wanaoombwa rushwa na
askari, kuondokana na usiri kwa kuwafichua hata baada ya kuwapatia fedha.
"Kama
askari akikuomba fedha zozote ni vizuri umpatie kama unazo. Na baada ya hapo,
njoo utoe taarifa kwangu nami nitakurejeshea fedha hizo,” alisisitiza Mpinga akisisitiza kwamba wanao wapelelezi wa
kubaini ukweli juu ya tuhuma dhidi ya askari wao.
Akilenga
kujibu malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na waendesha
bodaboda dhidi ya baadhi ya askari wa usalama barabarani, Mpinga alisisitiza, “kikubwa
hapa ni ushirikiano wa kila upande, utakaowezesha tabia hii kukoma."
Akizungumzia
maboresho katika mifumo ya utendaji kazi wa kikosi hicho, Mpinga alisema
yamesaidia kupunguza ajali za barabarani kuanzia Januari mwaka huu
tofauti na kipindi kama hicho, mwaka jana.
Takwimu
alizotoa kwa waandishi wa habari zinaonesha Januari hadi Juni kumekuwa na
ajali 2,096, vifo vinne na majeruhi 2,366 wakati mwaka jana, katika
kipindi kama hicho, ajali zilikuwa 11,311, vifo 1,739 na majeruhi 9,889.
Mkoa wa
Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na ajali nyingi ambazo ni 5,052 sawa na
asilimia 60.2 ya ajali zote.
Kamanda
Mpinga alisema katika utekelezaji wa kupunguza ajali hizo, wameimarisha
kitengo cha utoaji elimu kwa umma na kuboresha programu za luninga na
redio kutoa uelewa kwa wananchi.
Credit: Habari leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRAFIKI 27 WATIMULIWA KAZI KWA KULA RUSHWA.”
Post a Comment