Friday, July 18, 2014
WINDO LA MBEYA CITY FC KUELEKEA LIGI KUU NI `MOTO WA KUOTEA MBALI`.
Do you like this story?
WAGONGA nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc wapo katika
mkakati mzito wa kurejea na nguvu mpya kwenye michuano ya ligi kuu, msimu wa
2014/2015 unaotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Klabu hiyo inayonolewa na kocha maarufu nchini na
kocha bora wa msimu uliopita, Juma Mwambusi ina nia ya kutwaa ubingwa msimu
ujao baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika msimu wake wa kwanza.
Ikiwa ni sehemu ya kujiweka sawa, Mbeya City fc
itacheza mechi za kirafiki za kimataifa nchini Malawi na Zambia .
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mussa Mapunda
alisema wanatarajia kucheza angalau mechi mbili za kirafiki za kimataifa nchini
Zambia kabla ya kwenda Malawi kwa maandalizi zaidi.
“Malengo yetu ni kutwaa ubingwa msimu ujao. Nina
uhakika tutaweza kufanikiwa”. Alisema Mapunda.
Mapunda alisema maamuzi ya kuweka kambi nchi
jirani yamechagizwa na kitendo cha shirikisho la soka Tanzania kusogeza
ligi mbele mpaka septemba 20 mwaka huu.
Kwa upande wake, kocha Juma Mwambusi alisema
amepanga programu nzuri ya mazoezi kwa vijana wake, na anaamini watafanya kazi
nzuri msimu ujao.
Mwambusi alisema kikosi chake hakijabadilika sana
kwasababu karibu wachezaji wote wamebaki, achilia mbali wachache walioongezwa
akiwemo Them Ferlix `Mnyama` kutoka klabu ya Kagera Sugar.
“Malengo yetu ni kufanya vizuri zaidi ya msimu
uliopita. Tunajiandaa vizuri ili kukabiliana na changamoto iliyopo mbele yetu”.
Alisema Mwambusi.
Msimu uliopita, Mbeya City ilimaliza katika nafasi
ya tatu kwa kujikusanyia pointi 49. Walifungwa michezo mitatu tu.
Walifungwa bao 1-0 na Yanga katika dimba la Taifa,
wakafungwa 2-0 na Coastal Union, Mkwakwani Tanga na mechi ya mwisho kufungwa ni
dhidi ya mabingwa Azam fc ambapo walilala mabao 2-1 katika uwanja wao wa
nyumbani wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WINDO LA MBEYA CITY FC KUELEKEA LIGI KUU NI `MOTO WA KUOTEA MBALI`.”
Post a Comment