Friday, July 18, 2014
HII NDIO KAULI YA `MAJEMBE` YA TAIFA STARS KUELEKEA MECHI DHIDI YA `BLACK MAMBAS`.
Do you like this story?
TAIFA Stars chini ya kocha, Mholanzi,
Mart Nooij, inakabiliwa na mechi muhimu dhidi ya Msumbiji `Black Mambas` ,
kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kwenda kushiriki fainali za
mataifa ya Afrika, AFCON , mwakani nchini Morocco.
Mechi hiyo ya kwanza itapigwa
jumapili (julai 20 mwaka huu) ndani ya uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam , ambapo Stars watalazimika kupata ushindi wa mabao angalau 3-0
ili kujiweka mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mechi ya marudiano
itakayochezwa wiki mbili baadaye mjini Maputo nchini Msumbiji.
Kuelekea katika mechi hiyo ya
jumapili, unaweza kusema kikosi cha Taifa Stars kipo kamili gado kwasababu
nyota wake wote wa ndani na nje wapo tayari kwa kazi.
Mwinyi Kazimoto Mwitula alitua jana
asubuhi akitokea nchini Qatar anakocheza soka la kulipwa tayari kwa kuongeza
nguvu katika kikosi cha Stars.
Uzoefu wa Mwinyi katika soka la
kimataifa utasaidia sana kuimarisha safu ya kiungo itakayomkosa Frank Domayo
`Chumvi` kwasababu ni majeruhi.
`Majembe` mawili ya Stars yanayokipiga
TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu yapo nchini
tangu juzi.
Kuelekea katika mechi hiyo, Mart
Nooij ana wigo mpana wa kuamua nani aanze katika safu ya ushambuliaji.
Samatta amesema kwa upande wake,
maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na amefurahi kwasababu ni mzima wa afya
tofauti ni ilivyokuwa kwa mechi iliyopita mjini Harare nchini Zimbabwe.
“Maandilizi kwa mimi kama mimi
yako vizuri , kwasababu tulikuwa katika maandalizi ya ligi ya mabingwa,
tulikuwa tunafanya mazoezi magumu. Kwahiyo maandalizi yako vizuri kwangu na kwa
Thomas pia”. Alisema Samatta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HII NDIO KAULI YA `MAJEMBE` YA TAIFA STARS KUELEKEA MECHI DHIDI YA `BLACK MAMBAS`.”
Post a Comment