Friday, July 18, 2014
KIINGILIO CHA MECHI YA STARS, MSUMBIJI CHATAJWA 7,000/- VITI MAALUM (VIP) 30,000/-.
Do you like this story?
BONIFACE
WAMBURA
Viingilio kwa mechi ya Taifa Stars na Msumbiji
itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni sh.
7,000 na sh. 30,000 kwa viti maalumu 4,500 tu.
Kuanzia kesho asubuhi (Jumamosi) tiketi za
kielektroniki zitauzwa pia katika magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni
Shell, Dar Live Mbagala, Ferry Magogoni, Kigamboni, OilCom Chang’ombe, OilCom
Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa (Kariakoo), TCC Club Chang’ombe na
Uwanja wa Taifa.
Aidha tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga
*150*00# kisha bonyeza 4, bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni
173399 kisha ingiza 7000 kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena
7000 kwenye weka kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza 1
kukubali.
Utapokea
ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo vya kuchukua tiketi ukiwa na namba
ya uhakiki wa malipo yako.
Vituo vya MaxMalipo vya kuchukulia tiketi
ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket
(Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer
Illussions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN
Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).
Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop
Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen
Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori,
Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa
Taifa) na Uwanja wa Karume.
SEMINA ELEKEZI AIRTEL RISING STARS
Semina elekezi ya michuano ya Airtel
Rising Stars kwa mikoa sita inafanyika kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi
kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ni kutoka mikoa
ya Mbeya (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Mwanza (Katibu na mwakilishi wa
wanawake), Morogoro (Katibu), Ilala (Katibu na mwakilishi wa wanawake).
Temeke (Katibu na mwakilishi wa wanawake),
Kinondoni (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Dar es Salaam (Mwenyekiti na
Katibu), na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kitakachowakilishwa na
mwakilishi wa wanawake.
Washiriki wengine katika semina hiyo
ambayo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ni wajumbe wa
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya TFF.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIINGILIO CHA MECHI YA STARS, MSUMBIJI CHATAJWA 7,000/- VITI MAALUM (VIP) 30,000/-.”
Post a Comment