Friday, July 18, 2014
WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA WATAKIWA KUWA NA MTAZAMO MPYA UTAKAOWEZESHA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA.
Do you like this story?
Kiongozi wa Shule Kuu ya Sheria nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba alisisitiza suala la wanasiasa kurudi bungeni na kuhakikisha katiba mpya inapatikana. |
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo. |
Ushauri Umetolewa kwa
Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba kuwa na Mtazamo mpya utakaoiletea nchi
maslahi pindi watakaporudi bungeni katika mchakato wakutafuta katiba mpya
unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Hata hivyo kundi la Umoja
wa katiba ya wananchi (UKAWA) limezidi kushauri wakirudi bungeni na kuendelea
na majadiliano kwa msingi wa rasimu ya katiba.
Hayo yamesemwa jijini Dar
es Salaam jana Julai 17, 2014 na mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus
Kibamba ambapo ameeleza kwamba wabunge wanatakiwa kuachana na mtazamo wa
kisiasa pamoja na lugha zisizo na staa kwenye bunge hilo kwani wanatakiwa
kuzingatia uzalendo kwanza.
Aidha Bw. Kibamba amesema
kwamba licha ya muda kuwa mfupi kuelekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 wao
wanapendekeza juhudi zaidi zifanyike ili kukamilisha upatikanaji wa katiba
hiyo.
Naye Kiongozi wa shule kuu
ya Sheria nchini Kenya Profesa Patrick Lumumba amewasihi wanasiasa wa nchini
kuhakikisha katiba inapatikana kutokana na matakwa ya wananchi kwani nchini
jirani zimekuwa zikiiga mambo mengi kutoka huku.Bunge Maalum la katiba
linatajiwa kuanza tena Agosti 5, 2014 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA WATAKIWA KUWA NA MTAZAMO MPYA UTAKAOWEZESHA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA.”
Post a Comment