Friday, July 18, 2014
MAUAJI YA KUTISHA MKOANI KILIMANJARO, KIJANA AMPASUA KICHWA MTOTO NA KULA UBONGO WAKE, MWENYEWE AJIKATA UUME WAKE HADI KUFA
Do you like this story?
MAUAJI ya kutisha yanaendelea kuuandama
mkoa wa Kilimanjaro, baada ya kijana Laurance Flavian (20), mkazi wa Marangu
Mashariki kumuua Mwanafunzi wa darasa la Pili katika Shule ya Msingi Marangu
Hills, Francis Fortunatus (9), kwa kumkata mapanga sehemu za kichwani na kula
ubongo wake, kisha na yeye kujikata uume wake na kusababisha mauaji hayo.
Akizungumza Kamanda wa polisi mkoani
humo, Robert Boaz, amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Julai 18, 2014
saa7:15 asubuhi katika eneo la Marangu Pentekoste katika Wilaya ya Moshi mkoani
humo.
Amesema mtoto huyo ambaye pia ni
mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Marangu Hills alikutwa na
mauti wakati akielekea shuleni na kuwa kijana huyo (Laurance Flaviani), alianza
kumshambulia kwa kumkata na mapanga sehemu za kichwani nakutoa ubongo wake na
kuula hali iliyomsababishia, kufariki dunia papo hapo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Boaz,
kijana huyo baada ya kumuua mtoto huyo nayeye alijijeruhi kwa kuukata uume
wake, na kukimbizwa katika Hospitali ya Kilema ambapo alikufa wakati akipatiwa
matibabu kutokana na dutokwa na damu nyingi kaatika sehemu aliyojikata.
“Mtoto huyu akielekea shuleni asubuhi
ghafla kijana huyo ambaye nay eye sasa ni marehemu, alianza kumshambulia kwa
kumkata kwa panga kichwani bila sababu yeyote, hali iliyosababisha kifo
cha mtoto huyo papo hapo”alisema Kamanda Boaz.
Aidha, amesema chanzo cha mauaji hayo
hakijajulikana na kuwa taarifa za awali kuhusu tukio hilo kinasadikiwa kuwa
kijana huyo alikuwa na ugonjwa wa akili na kwamba kabla ya kutenda tukio hilo
alikuwa akifanya vurugu na kuvunja vioo vya nyumba yao za watu katika eneo
hilo.
Mashuhuda wasimulia Hata hivyo,
taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kijana huyo baada ya kutekeleza mauaji
hayo ambapo inadaiwa mtoto aliyemuua ni mtoto wa bosi wake wake na kwamba baada
ya kuukata uume wake alianza kuula kama nyama choma huku akikata kipande kimoja
baada ya kingine.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,
Tetrula Kimario, amesema kijana huyo ambaye alikuwa akifanya kazi ya
kutengeneza Sanamu za mapambo katika kiwanda kilichopo Marangu Pentekoste, na
kuwa Julai 17, 2014 alianza kubadilika kwa kufanya vitu visivyoeleweka ambapo
tajiri yake ambaye ni Baba wa mtoto aliyeuawa alimchukua na kumrudisha nyumbani
kwao karibu na alipokuwa anaishi mwanzoni.
Amesema, ilipofika leo asubuhi mtoto wa
bosi wake alitoka kwenda shule, ndipo kijana huyo alipomkata kichwa na kisha
kuanza kula ubongo wake, ambapo watu walifikia katika eneo la tukio waliamua
kumpiga kwa mawe hadi polisi walipofika katika eneo la tukio.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, mkoa huo
umekumbwa na matukio ya mauaji na unyanyasaji wa watoto waliochini ya umri wa
miaka kumi na nane (18)
chanzo:fikrapevu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAUAJI YA KUTISHA MKOANI KILIMANJARO, KIJANA AMPASUA KICHWA MTOTO NA KULA UBONGO WAKE, MWENYEWE AJIKATA UUME WAKE HADI KUFA”
Post a Comment