Sunday, July 27, 2014
HII HAPA NDIYO RATIBA YA SWALA YA SIKUKUU YA IDD EL FITRI.
Do you like this story?
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum ametangaza Swala ya Sikukuu ya Idd El Fitri
inayotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa wake.
Akizungumza na waandishi wa habari
kwenye kikao maalumu katika Ofisi za Mkoa wa Dar es Salaam za Baraza Kuu
la Waislamu (BAKWATA) jana, Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo sambamba na
hotuba mbalimbali inatarajiwa kufanyika saa moja asubuhi katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar kutegemea na siku ya Idd itakapodondokea ambapo
inatarajiwa kuwa siku ya Jumatatu Julai 28 au Jumanne Julai 29 mwaka huu.
Shekhe Alhad alisema kuwa swala
hiyo itahudhuriwa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete na
viongozi mbalimbali wa Kiislamu na wa kitaifa ikifuatiwa na Baraza la Idd
litakalofanyika saa 9 Alasiri katika Viwanja vya Karimjee, Dar ambapo Mgeni
Rasmi wa Baraza hilo atakuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda.
VIA>>
MALUNDE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HII HAPA NDIYO RATIBA YA SWALA YA SIKUKUU YA IDD EL FITRI.”
Post a Comment