Saturday, July 12, 2014
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LATOA TAARIFA KUHUSIANA NA HALI YA UHALIFU KWA KIPINDI CHA NUSU MWAKA JAN-JUN 2014
Do you like this story?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya( SACP) Ahmed Msangi akitoa Taarifa kwa waandishi wa Habari. |
Waandishi wa habari wakiwa makini kusikiliza Taarifa ya Uhalifu katika Mkoa wa Mbeya. |
Kwa
ujumla hali ya uhalifu mkoa wa mbeya kwa kipindi cha jan- juni, 2014
ilikuwa shwari. Aidha makosa mbalimbali yaliripotiwa kutokea ikiwa ni pamoja na
mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha/nguvu, kubaka, uvunjaji, wizi wa mifugo,
pikipiki n.k. hata hivyo watuhumiwa mbalimbali walikamatwa na kufikishwa
mahakamani ambapo baadhi ya kesi zimemalizika na nyingine zipo katika
hatua mbalimbali.
Katika
kipindi cha jan-juni, 2014 Jumla ya makosa yote ya jinai yaliyoripotiwa
kutokea yalikuwa 13,481, ikilinganishwa na matukio 13,670
yaliyoripotiwa kutokea kipindi kama hicho mwaka 2013, hivyo kuna pungufu
ya matukio 189, sawa na asilimia 2 [2%].
Kwa
upande wa makosa ya usalama barabarani Jumla ya matukio yote
yaliyoripotiwa katika kipindi cha jan-juni, 2014 ikiwemo matukio
ya ajali na ukiukwaji wa sheria za Usalama barabarani na usafirishaji yalikuwa 26,668
wakati kipindi kama hicho mwaka 2013 yalikuwa 25,266 hivyo kuna ongezeko
la matukio 1,402 sawa na asilimia 4 [4%] matukio ya ajali
yaliyoripotiwa kipindi cha jan-juni 2014 yalikuwa 197 wakati
kipindi kama hicho mwaka 2013 yalikuwa 266 hivyo kuna pungufu
ya matukio 69 sawa na asilimia 26 [26%].
Ajali
za vifo zilizoripotiwa kipindi cha jan-juni 2014 zilikuwa 112
wakati kipindi kama hicho mwaka 2013 zilikuwa 128 hivyo kuna pungufu
ya matukio 16 sawa na asilimia 13 [13%]. Watu waliokufa kipindi
cha jan-juni 2014 walikuwa 130 wakati kipindi kama hicho mwaka 2013
walikuwa 157 hivyo kuna pungufu ya watu 27 sawa na
asilimia 18 [18%].
Ajali
za majeruhi zilizoripotiwa kipindi cha jan-juni 2014 zilikuwa 85 wakati
mwaka 2013 zilikuwa 138 hivyo kuna pungufu ya ajali 53
sawa na asilimia 39 [39%]. Watu waliojeruhiwa jan-juni 2014
walikuwa 245 wakati kipindi kama hicho mwaka 2013 walikuwa 455
hivyo kuna pungufu ya watu 210 sawa na asilimia 47 [47%].
Makosa
ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji katika kipindi cha
jan-juni 2014 yalikuwa 26,471 wakati kipindi kama
hicho mwaka 2013 yalikuwa 24,967 hivyo kuna ongezeko la
makosa 1,504 sawa na Asilimia 6 [6%]. Tozo lililokusanywa kutoka
kwa makosa [notification] kwa kipindi cha jan-juni 2014 lilikuwa tshs
705,780,000/= ikilinganishwa na tshs 654,740,000/= kipindi kama
hicho mwaka 2013 hivyo kuna ongezeko la tshs 51,040,000/=,
sawa na asilimia 8 [8%], hivyo kuufanya mkoa wa mbeya kuwa miongoni mwa
mikoa iliyoongoza kwa ukusanyaji tozo nchini.
Makosa
kero kwa jamii.
Jumla
ya matukio ambayo ni kero kwa Jamii yaliyoripotiwa Mkoa wa Mbeya kwa
kipindi cha jan-juni 2014 yalikuwa 2,567 wakati kipindi kama
hicho mwaka 2013 yalikuwa 2,683 hivyo kuna pungufu
ya matukio 116 sawa na asilimia 5 [5%].
Katika
kipindi cha jan-juni 2014, matukio ya mauaji yalikuwa 135 wakati
mwaka 2013 yalikuwa 156 kuna pungufu ya matukio 21 sawa na
asilimia 14 [14%], kubaka jan-juni 2014 yalikuwa 252 mwaka
2013 yalikuwa 197 hivyo kuna ongezeko la matukio 55
sawa na asilimia 28 [28%].
Matukio
ya unyang’anyi wa kutumia silaha jan-juni 2014 yalikuwa 4 mwaka 2013
yalikuwa 5 kuna pungufu ya tukio 1,sawa na asilimia 20.unyang’anyi
wa kutumia nguvu jan-juni 2014 yalikuwa 61 mwaka 2013
yalikuwa 89 kuna pungufu ya matukio 28,sawa na
asilimia 32 [32%].
Matukio
ya uvunjaji jan-juni 2014 yalikuwa 180, mwaka 2013
yalikuwa 202, kuna pungufu ya matukio 22, sawa na asilimia
11. Wizi wa mifugo jan-juni 2014 yalikuwa 126, mwaka 2013
yalikuwa 102, kuna ongezeko la matukio 24, sawa na
asilimia 24 [24%]. Wizi wa pikipiki jan-juni 2014 yalikuwa 96 mwaka
2013 yalikuwa 69, kuna ongezeko la matukio 27, sawa
na asilimia 40. Matukio ya wizi jan-juni 2014 yalikuwa 1,713
mwaka 2013 yalikuwa 1,863 yalikuwa 150, sawa na asilimia 8
[8%].
Matukio
yatokanayo na jitihada za jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau na wananchi
wengine.
Jumla
ya makosa 282 yaliripotiwa kipindi cha jan-juni,2014,
ikilinganishwa na matukio 244, mwaka 2013, hivyo kuna ongezeko la
matukio 38, sawa na asilimia 16 [16%].
Matukio
ya kupatikana na bhangi jan-juni 2014 yalikuwa 130, mwaka 2013
yalikuwa 124, hivyo kuna ongezeko la matukio 6, sawa na
asilimia 5. Pombe ya moshi [gongo] jan-juni 2014 yalikuwa 86,
kipindi kama hicho mwaka 2013 yalikuwa 50, kuna ongezeko
la matukio 36, sawa na asilimia 72. Kupatikana na silaha jan-juni
2014 yalikuwa 19, kipindi kama hicho mwaka 2013 yalikuwa 15,
kuna ongezeko la matukio 4, sawa na asilimia 27 [27%].
Matukio
ya kukamatwa wahamiaji Haramu jan-juni 2014 yalikuwa 14, kipindi
kama hicho mwaka 2013 yalikuwa 36, kuna pungufu
ya matukio 22, sawa na asilimia 62 [62%]. Kupatikana
na nyara za serikali jan-juni 2014 yalikuwa 8, kipindi kama
hicho mwaka 2013 yalikuwa 12, kuna pungufu ya matukio 4,
sawa na asilimia 34 [34%]. Kupatikana na dawa za kulevya jan-juni
2014 yalikuwa 1, sawa na kipindi kama hicho mwaka 2013. Aidha
mafanikio haya yalitokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Jeshi la polisi,
wadau na wananchi mbalimbali.
Mafanikio.
Baadhi
ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:-
· kupungua
kwa uhalifu kwa asilimia 2.
· kupungua
kwa matukio ya mauaji yatokanayo na imani potofu za kishirikina,
kutoka matukio 32, jan- juni- 2013 na kufikia matukio 23, jan-juni,
2014, sawa na asilimia 29.
Jumla
ya wahamiaji haramu 195 walikamatwa wakiwemo:-
(i)
waethiopia - 152
(ii)
wasomalia - 10
(iii)
pakistan - 7
(iv)
burundi – 23
(v)
malawi – 2
(vi)
msumbiji 1.
·
Pombe haramu ya Moshi {gongo} yenye ujazo wa lita 479 pamoja na mitambo
16 ilikamatwa.
·
Bangi yenye uzito wa kgm 296 na gram 678, miche 314 pamoja na
mashamba matatu ya bhangi yenye ukubwa wa Jumla ya ekari moja na robo
yalikamatwa.
·
mirungi uzito wa gram 500 ilikamatwa.
· silaha
/bunduki 19 zilikamatwa kati ya hizo gobole 15, bastola 2 za
kienyeji, riffle 1 na s/gun 1. Pia silaha mbili zilikamatwa baada ya
majambazi kuuawa katika jaribio la kufanya unyany’anyi. Silaha hizo ni smg
n0-3514 na ak-47 n0- 592058 na risasi 25 kwenye magazine.
· Mafuta aina
ya diesel ujazo wa lita 3,265 mali ya wizi ilikamatwa.
· Nyara za
serikali zenye thamani ya tshs 1,700,000/= na usd 2,130
zilikamatwa.
Changamoto.
Pamoja
na mafanikio yaliyopatikana, lakini bado kuna changamoto zinazolikabili jeshi
la polisi mkoa wa mbeya. Miongoni mwa changamoto hizo ni:
- Bado baadhi ya wanachama wa vyama /viongozi wa siasa hawajaona umuhimu wa kutii sheria wao wenyewe na kuendelea kutoa maneno ya kuwagawa wananchi.
§ baadhi ya wananchi
wanaendelea kuficha wahalifu na uhalifu katika maeneo yao na kushindwa kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi.
§ bado makosa ya kubaka, wizi
wa mifugo na wizi wa pikipiki yameongezeka kipindi cha jan-juni, 2014
ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2013. Hata hivyo mikakati
inafanywa ili kupunguza/kudhibiti matukio hayo.
§ licha ya makosa
ya mauaji kupungua kutoka 156 jan - juni, 2013 na
kufikia 135 jan - juni, 2014, lakini matukio 23 yalitokana
na imani potofu za kishirikina [uchawi], matukio 33 yalitokana na
wananchi kujichukulia sheria Mkononi, matukio 16 yalitokana na ugomvi
majumbani, matukio 11 ugomvi vilabuni, matukio 20 wivu/ugoni,
matukio 9 kisasi na matukio 23 sababu nyinginezo.
Wito
wa kamanda:
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed z.
Msangi ninatoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi
hasa kwa kutoa taarifa za uhalifu/wahalifu mapema ili kuzuia matukio ya uhalifu
na kiuhalifu yasitokee.
Aidha
ninatoa wito kwa Wazazi/Walezi kuzingatia utoaji wa malezi bora kwa
watoto/vijana ili wakue katika misingi mizuri ya maadili mema kijamii na
kujiepusha na matukio ya kiuhalifu/kukataa uhalifu wangali wadogo ikiwa ni
pamoja na kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya, kucheza kamari n.k.
Halikadharika,
katika kuhakikisha uhalifu unapungua, Vyombo vya Habari vina nafasi yake katika
jamii ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa Elimu Mbalimbali za kiulinzi na
usalama kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali. Aidha kwa kutambua mazingira
tuliyonayo na changamoto zilizopo katika mkoa Wetu, kila mmoja wetu aone kila
sababu ya kufikisha ujumbe/taarifa yenye kukemea/kupinga na kuleta mabadiliko
chanya katika Jamii kwa lengo la kuleta amani na utulivu.
Kwa
kutambua kuwa suala la ulinzi na Usalama unaanzia ngazi ya familia, kijiji,
kitongoji, kata, Tarafa, Wilaya hadi ngazi ya Mkoa, ni vyema kila mmoja wetu
kutambua na kuamini usalama wa mali na maisha yetu unaanza na mimi, wewe na
sisi sote. Kwa kuimarisha ulinzi na Usalama wetu na mali zetu inatoa fursa kwa
wawekezaji kuwekeza katika mkoa wetu, wananchi kujiajiri na kuajiriwa ikiwa ni
pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii bila
kuathiri amani na utulivu.
Imetolewa
na:
[Ahmed
z. Msangi – sacp]
kamanda
wa polisi mkoa wa mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LATOA TAARIFA KUHUSIANA NA HALI YA UHALIFU KWA KIPINDI CHA NUSU MWAKA JAN-JUN 2014”
Post a Comment