Sunday, July 26, 2015
MWANAMUZIKI BONGO FLEVA KHADIJA SHABAN "KEISHA"ASHINDA CCM
Do you like this story?
MSANII wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya
'Keisha' ameibuka mshindi kwenye kura za maoni za Ubunge wa viti maalum kundi
la Walemavu MKoa wa Dodoma na kuwa mshindi wa kwanza.
Keisha amepata kura 340 huku Stella Fueda akiibuka na kura 112, Anna Fungo kura 100 na Graceana Kavishe kura 54.
Jumla ya kura 721 zilipigwa ambapo kura 75 ziliharibika na kura za halali zilikuwa 646.
Msanii huyo aliwahi kuhojiwa na vyombo vya
habari na kubainisha kuwa japo ni mlemavu wa ngozi lakini anajikubali
anajipenda kujiamini na amekuwa akipigania amani ambayo wanastahili kuipata
kutoka nchini.
Alisema alipoanza kuweka picha zake za siasa
kwenye mtandao kuna baadhi ya watu walimpongeza na wapo waliosema kuwa hana
uchungu na wenzake kwani waliamini anaingia kwenye siasa kwa nia ya
kujinufaisha “Wapo wanaohisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe
mimi
ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu” alisema.
Alisema fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole
kimoja hakivunji chawa akimaanisha kuwa lazuima kusimamia sheria ambazo
zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima kuwe na wawakilishi wa kutosha
ndani ya bunge ili sauti zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.
Taarifa ya Sifa Lubasi, Dodoma
Habari za asubuhi ndugu zangu rafiki zangu
mashabiki zangu na media zote nchini.najua wengi mnajiuliza maswali mengi sana
juu yangu kwanini nimeamua kuingia kwenye siasa lakini leo naomba nifunguke na
kuwaambia kitu.
Mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali
najipenda na ninajiamini lakini yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo
tunastahili kuipata kutoka nchini kwetu.
Nilipoanza kupost picha zangu za siasa kuna
ambao walinipongeza na kuna ambao walinisema kwamba sina uchungu na wenzangu
kwakuwa wanahisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni
mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu.fimbo ya
mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa nikimaanisha kwamba lazima
tusimamie sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima tuwe na
wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zetu zisikike ili sheria
kutungwa na kutekelezwa pia.hivyo mimi kama mtanzania mwenzenu nahitaji support
yenu ili niweze kufikia malengo yetu kwa yeyote ambaye anaupendo nasi na mimi
na harakati zangu anisaidie kwa chochote ambacho kitanifikisha nnapoataka.
this is my tigo no 0718785045 na hii ni
account number yangu ya crdb 011 2022295800 jina ni hadija shabani Taya unaweza
kuchangia humo na kwa upendo kabisa naomba u repost hii post kadri muwezavyo
ahsanteni shukrani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANAMUZIKI BONGO FLEVA KHADIJA SHABAN "KEISHA"ASHINDA CCM”
Post a Comment