Saturday, July 12, 2014
WASICHANA WABAKWA NA KUNYONGWA MKOANI LINDI
Do you like this story?
WASICHANA saba wamepoteza maisha
wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya kubakwa na kunyongwa kisha kuwekewa
vijiti na chupa kwenye sehemu zao za siri.
Wasichana hao wamepoteza maisha kwa
nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne iliyopita na wamekuwa wakipigiwa
simu nyakati za usiku na kukutana na waliwapigia simu ambapo hubakwa na
kunyongwa na kisha katika sehemu za siri kuwekewa vijiti au chupa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick
Mwananzila (PICHANI) amebainisha aina hiyo ya mauaji jana wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.
Mwananzila alikuwa amekwenda
hospitalini hapo kuwatazama majeruhi ambapo alifafanua kuwa mauaji hayo
yanaendelea na juzi mtu mwingine aliuawa katika mazingira hayo.
Alisema, "serikali ya wilaya
ilishatoa namba za simu kuwa unapopigiwa simu mtoto wa kike fanya juhudi
kumjulisha mwenzako au piga simu kituo cha polisi ili kuweza kukabiliana na
watu hao wanaotoa roho za watu".
Mwananzila alisema kuwa binti mmoja
aliweza kupigiwa simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu kituo cha polisi na
kuweka mtego baada yeye kutoka nje, polisi walikuwa wameshazingira maeneo hayo
na wauaji wale walimfuata ndipo huyo binti alianza kuvutana nao na hatimaye
Polisi waliwatia mbaroni watu hao. Mkuu huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na
kusema: “ni makosa kwa wasichana kutoka nje baada ya kupigiwa …
"kinachotakiwa kwanza mjulishe
mwenzako, lakini unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa
kike".
Alisema mauaji hayo yana ishara ya
imani ya kishirikina. Hata hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika. Alisema suala
hilo liko ndani ya uchunguzi hivyo ni vizuri kufanyia kazi kwanza na kuwataka
wananchi wawe na subira.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WASICHANA WABAKWA NA KUNYONGWA MKOANI LINDI ”
Post a Comment