Saturday, July 12, 2014

IGP ERNEST MANGU ATOA TAMKO KUHUSU MILIPUKO YA MABOMU NCHINI.



Mkuu wa jeshi la polisi nchini inspekta jenerali Ernest Mangu ametoa tamko kuhusu matukio ya ulipuaji wa mabomu na kusema  wananchi wasiwe na wasiwasi kwani jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na sasa lipo katika hatua nzuri ila wahakikishe wanatoa ushirikiano katika kuwafichua wahuska.

Akizunguza jinini Dar es Salaam katika mkutano uliowahusisha wakuu wa polisi kutoka katika nchi za kusini mwa Afrika, kamanda Mangu amesema jeshi lina kuna kichwa usiku na mchana kuwabaini wanaojihusisha na matukio hayo.

Kufuatia kauli hiyo baadhi ya wananchi wametoa maoni yao na kusema kuwa japo dhana kubwa iliyojengeka kwa jamii kuwa ulinzi na jukumu la polisi ni vyema sasa kila mwananchiashiriki kulinda amani na kulisaidia jeshi la polisi.

Awali mwenyekiti wa umoja wa wakuu wa polisi  kusini mwa Afrika  na amabaye ni mkuu wa jeshi la polisi nchini namibia amesema sababu kubwa za uhalifu  katika nchi  wanachama ni pamoja kutokuwepo na vifaa vya kisasa vya kufanya  uchunguzi hasa katika usafirishaji wa madawa ya kulevya .

0 Responses to “IGP ERNEST MANGU ATOA TAMKO KUHUSU MILIPUKO YA MABOMU NCHINI.”

Post a Comment

More to Read