Tuesday, July 22, 2014
KHAMIS KIIZA ‘DIEGO’ APIGWA CHINI YANGA SC, OKWI KUENDELEA KUWIKA!.
Do you like this story?
KLABU ya Yanga imembwaga mshambuliaji
wake Mganda, Khamis Kiiza ‘Diego wa Kampala’ baada ya kusajiliwa kwa Wabrazil
wawili, Andrey Coutinho na Geilson Santos Santana `Jaja`.
Baada ya Jaja kusaini mkataba wa miaka
miwili jana makao makuu ya klabu ya Yanga, kulikuwa na utata ni mchezaji gani
atapigwa chini kati ya Kiiza na Emmanuel Anord Okwi.
Awali ujio wa Jaja ulielezwa kuwaweka
kitimoto Kiiza na Okwi, huku mmojawapo akitakiwa kutolewa kafara.
Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu
umezipata ni kwamba kocha Maximo amependekeza kuachwa kwa Kiiza kutokana na
ripoti iliyoachwa na Hans Van Der Pluijm.
Mzigo huo uliofuatwa chini ya kapeti
unasema kuwa Pluijm katika ripoti yake aliyowasilisha kwa viongozi baada ya
kumalizika kwa msimu uliopita, alisema ili Emmanuel Okwi acheze Yanga sc,
lazima Kiiza aondolewe.
Kwa kuzingatia mapendekezo hayo, Maximo
amefuata ushauri huo na sasa Kiiza rasmi anaondoka Jangwani.
Katika hatua nyingine, imeelezwa na
chanzo cha uhakika kuwa Maximo amewabana viongozi wa Yanga akiwataka wajenge
uwanja wa mazoezi wa Kaunda ili kuepukana na adhaa anayoipata.
Maximo amewakazia na amesema hakuna
jinsi, lazima uwanja huo ujengwe muda huu.
Pia amewataka viongozi kuboresha vyumba
vya jengo la Jangwani ili wachezaji wote waishe pale.
Taarifa zinasema, Maximo amesema
haiwezekani timu kukaa saa mbili kwenye foleni inapoelekea uwanjani na kurudi
kambini.
Kwa mazingira hayo anataka wachezaji
wake wakae makao makuu ya Yanga, mitaa ya Twiga na Jangwani, halafu
uwanja wa Kaunda ujengwe.
Mbrazil, Marcio Maximo anafahamika kwa
kuwa na msimamo mkali katika mambo yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KHAMIS KIIZA ‘DIEGO’ APIGWA CHINI YANGA SC, OKWI KUENDELEA KUWIKA!.”
Post a Comment