Sunday, July 13, 2014
KUWAONA `MADOGO` WA SERENGETI BOYS KIINGILIO HELA YA MBOGA TU!
Do you like this story?
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Mechi ya
kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika Kusini (Amajimbos)
itachezwa kwa kiingilio cha sh. 2,000.
Uwanja wa
Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam ndiyo utakaokuwa mwenyeji wa mechi
hiyo itakayochezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri.
Waamuzi
wa mechi hiyo wanatoka Shelisheli. Mwamuzi wa kati ni Allister Barra wakati
wasaidizi wake ni Gerard Pool na Jean Joseph Felix Ernest wakati mezani atakuwa
Nelson Emile Fred.
Kamishna
wa mechi hiyo atakuwa Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.
Kikosi
cha Serengeti Boys chini ya kocha Hababuu Ali Omari kipo kambini kwa zaidi ya
wiki mbili sasa kikijiandaa kwa mechi hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati
ya Agosti 1 na 3 nchini Afrika Kusini.
Wakati
huo huo, Alfred Kishongole Rwiza wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi
ya marudiano ya michuano hiyo ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17
kati ya Rwanda na Uganda.
Mechi
hiyo itachezwa nchini Rwanda kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu. Waamuzi wa mechi
hiyo watatoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUWAONA `MADOGO` WA SERENGETI BOYS KIINGILIO HELA YA MBOGA TU!”
Post a Comment