Monday, July 7, 2014
MADAM RITHA AELEZEA JINSI ALIVYOTESEKA KWA SIKU 365.
Do you like this story?
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Benchmark Productions inayoendesha shindano la kusaka vipaji vya muziki, Bongo
Star Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam’ amesimulia mateso aliyopitia takriban
mwaka sasa (siku 365) baada kuvunjika mguu mwaka jana alipopata ajali ya gari
katikati ya Jiji la Dar.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum
hivi karibuni aliponaswa na gongo linalomsaidia kutembea, Madam Rita alisema
kwa kusikitisha kwamba, baada ya kupata ajali alitibiwa kwenye Hospitali ya Muhimbili
lakini madaktari walimwambia aliteguka tu kumbe alikuwa amevunjika mfupa.
“Nimepitia mateso makubwa. Mwaka jana
baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu nilipopelekwa Muhimbili waliniambia
nimeteguka tu, na wakaamua kunifunga hogo ambalo baadaye walinifungua na
kuniambia nimepona,” alisimulia Madam Rita na kuongeza:
“Baada ya pale nilianza kujiachia hata
niliposikia maumivu na kuwaambia walisema niukanyagie tu kwamba hali hiyo
ingebadilika kwa sababu ulielekea kupona, kumbe nilikuwa nimevunjika kabisa
mfupa na kama ningejua siku nyingi hata nisingejiumiza kiasi hicho.
“Ujue baada ya kuambiwa hivyo,
nilishangaa kuona maumivu yanazidi, nikaamua kwenda nchini Afrika Kusini kwa
ajili ya kuuangalia zaidi mguu wangu kwa sababu maumivu yalikuwa yakiongezeka
kila siku.
“Nilikwenda kwenye Hospitali ya Morning Site ya Afrika Kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na kugundulika nilivunjika mfupa na kwamba tayari nilipokuwa nikitembea ilikuwa ikipandiana.“Ona sasa nilivyoteswa na mguu huu maana ajali nilipata mwaka jana na huu upasuaji nimefanyiwa mwaka huu Afrika Kusini.
“Kiukweli hospitali zetu saa nyingine
zinatusababishia shida ambazo siyo za lazima maana kama awali wangenifanyia
upasuaji wakati nawaambia ninaumia baada ya kunitoa hogo, basi leo ningekuwa
nafanya shughuli zangu.
“Naona bora pale Fame Centre (Dar)
maana wao waligundua tatizo na kunishauri kwenda Sauzi ambapo nimefanyiwa
upasuaji na mguu unaelekea kupona kwa sababu mwanzo nilikuwa natumia magongo
mawili lakini ona leo ninajikongoja kwa gongo moja ambalo nalo si muhimu sana
sasa.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MADAM RITHA AELEZEA JINSI ALIVYOTESEKA KWA SIKU 365. ”
Post a Comment