Monday, July 7, 2014
WASICHANA 60 WAKWEPA BOKO HARAM.
Do you like this story?
Maafisa
wa usalama wa Nigeria wamesema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa
umri mdogo wamekewpa kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamewateka
nyara.
Wanawake
hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu
na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.serikali ya Nigeria
imeitisha kufanywe uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
Baadhi
ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka
siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa Ijumaa hiyo (4 Julai) walifanikiwa
kuwaua wapiganaji zaidi ya 50 karibu na mji wa Damboa.
Hata
hivyo bado wanamgambo hao wa Boko Haram wanawazuilia zaidi ya wasichana wengine
200 waliowateka nyara mwezi Aprili. Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya
kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa
wakijitolea kuisaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WASICHANA 60 WAKWEPA BOKO HARAM.”
Post a Comment