Monday, July 7, 2014
MAXIMO AAHIDI NEEMA.
Do you like this story?
Kocha
wa Yanga, Marcio Maximo amewatoa hofu nyota wake kwa kuwaahidi kupigania
masilahi mazuri kwa kila mmoja, wakati wachezaji hao wakisotea mishahara yao ya
mwezi uliopita.
Maximo
aliwaambia wachezaji wake baada ya mazoezi ya juzi asubuhi kwenye Uwanja wa
Loyola jijini Dar es Salaam kuwa yeye ni mmoja wa watu wanaopigania masilahi ya
wachezaji na wiki iliyopita alikutana na mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji
na kuzungumza naye kuhusu jambo hilo hivyo amewataka wachezaji wake wacheze
mpira na kuhusu masilahi wasiwe na shaka.
“Nimekuwa
nikipigania masilahi mazuri ya wachezaji tangu nikiwa na timu ya Taifa
‘Taifa Stars’ na nataka kufanya hivyo hata nikiwa hapa, lakini muhimu ni
kunihakikishia kuwa mtajituma uwanjani na kujitolea na mnithibitishie
hilo.
“Nimeongea
na Manji kuhusu jambo hilo na msiwe na wasiwasi kila mmoja wenu atapata
masilahi mazuri na kufurahia soka, lakini hakikisheni mnajituma uwanjani na
kufanya vizuri na ndipo kila kitu kitakwenda vizuri upande wenu,” alisema
Maximo.
Hata
hivyo; licha ya Maximo kutoa tumaini hilo kwa wachezaji wake, lakini upande wa
pili wachezaji hao wamelalamikia kutopata mishahara yao ya mwezi uliopita mpaka
sasa jambo ambalo linawaweka katika wakati mgumu katika mazoezi yao.
Wachezaji
hao wamedai kuwa wanategemea mshahara huo kwa ajili ya kujikimu mahitaji
mbalimbali kama chakula na usafiri, lakini wanashangazwa na ukimya wa
viongozi wao hadi sasa.
“Ukweli
hali ni mbaya tunafanya tu mazoezi kwa kuwaheshimu viongozi, lakini wengi
hatuna fedha na hatujui tutapata lini na kama unavyojua tunategemea mshahara
kwa ajili ya chakula na usafiri, na mazoezi yenyewe magumu sasa hata
hatujui tutaishije halafu ni bora hata tungekuwa tunapata posho, basi mshahara
tusingekuwa na haja nao lakini hakuna kitu tunachopata,” walidai wachezaji hao
huku wakiombwa wasiandikwe majina yao gazetini.
Inadaiwa
kuwa nyota wa timu hiyo wakiongozwa na Mrisho Ngasa na Mbuyu Twite mara
nyingine hawatokei katika mazoezi hayo na hata wakitokea wamekuwa wakifanya
chini ya kiwango kutokana na jambo hilo la kutopata mshahara kuwaumiza.
Juzi
katika mazoezi yaliyofanyika Loyola wachezaji hao hawakutokea huku kocha
wao Maximo aking’aka kwani hawakumpa taarifa zao za kukacha
mazoezi na wala hawakutoa taarifa yoyote kwa viongozi.
Wachezaji
wa Yanga hawapewi posho za mazoezi baada ya viongozi wa Yanga kudai nyota hao
wanalipwa mishahara mikubwa tofauti na timu nyingine.
Kwa
sasa Azam ndiyo inayolipa wachezaji wake mishahara mikubwa ikifuatiwa na Yanga
na Simba inashika nafasi ya tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAXIMO AAHIDI NEEMA.”
Post a Comment