Tuesday, July 8, 2014
MAJANGA: MOTO WATEKETEZA GEREZA.
Do you like this story?
Moto mkubwa umeteketeza gereza la
Nyakiriba lililoko Magharibi mwa Rwanda, katika wilaya ya Rubavu, karibu na
mpaka wa DRC.
Tukio hilo limeripotiwa kutokea
Jumatatu (July 7) ambapo watu watatu wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 40
wamejeruhiwa vibaya kutokana na moto huo.
Akiongea, Mkuu wa wilaya ya Rubavu,
Sheikh Hassan Bahame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa
waliopoteza maisha ni mahabusu watatu na kwamba majeruhi 44 walikimbizwa
hospitali kuu ya wilaya kupata matibabu.
Amesema ilikuwa vigumu kwa jeshi la
zima moto kutekeleza kazi yake ipasavyo kutokana na mazingira ya gereza hilo
kuwa mlimani hali iliyopelekea vitu vingi kuteketea.
Mkuu huyo wa wilaya alieleza kuwa bado
hawajafahamu chanzo na thamani ya vitu vilivyoteketea katika tukio hilo.
Tuio hili linatokea mwezi mmoja baada
ya gereza jingine la Muhanga kuteketea kwa moto katika jimbo lililopo kusini
mwa Rwanda.
Tayari uchunguzi umeanza juu ya matukio
hayo yote mawili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAJANGA: MOTO WATEKETEZA GEREZA.”
Post a Comment