Tuesday, July 8, 2014
BOMU LALIPUKA ARUSHA KATIKA MGAHAWA WA TRADITIONAL INDIAN CUSINE NANE WAJERULIWA
Do you like this story?
Mlipuko unaosadikiwa ni bomu
umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha katika mgahawa wa
Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na
kujeruhi watu nane
Akithibitisha kupokea wagonjwa
walioadhiriwa na bomu hilo Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya
Seliani Dr. Paulo Kisanga alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira yasaa
4:30 usiku katika eneo kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia
majira ya saa tano kasoro na saatano .
Alisema kuwa walipokea wagonjwa
nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika
wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu
ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.
“kati yawagonjwa hao nane mmoja
alitwa akiwa mahututi sana kwani mguu wake ulikuwa umeadhiriwa sana na bomu
hiloivyo ikatulazimu kumkata mguu mmoja wa kushoto ,kwakweli mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa Deepak
Gupta (25) mwanaume na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupokatika chumba
cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani”alisema Kisanga
Alisema kuwa katika majeruhi
au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na
kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya
uangalizi wa madaktari
Aidha aliwataja majeruhi hao kwa
majina kuwa ni pamoja na Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj
Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42)
pamoja na Deepak Gupta (25) wote wakiwa na asili ya kiasia
Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa
wagonjwa hao walio waliofika hapo hospitali walidai kuwa bomu
hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BOMU LALIPUKA ARUSHA KATIKA MGAHAWA WA TRADITIONAL INDIAN CUSINE NANE WAJERULIWA ”
Post a Comment