Wednesday, July 9, 2014
HAYA NDIO MANENO ALIYOTAMKA LUIZ FELIPE SCOLARI BAADA YA KUFUNGWA 7-1 NA UJERUMANI
Do you like this story?
Luiz Felipe Scolari,
kocha wa Brazil
"Ni wakati mbaya zaidi
kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na siku mbaya zaidi katika maisha
yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea. Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni
mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini
mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.
Lilikuwa chaguo langu.
Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo, tulicheza kwa kiwango chetu cha
mwisho-lakini tumeishia dhidi ya timu kubwa ya Ujerumani. Hatukukata tamaa na
kurudi nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada ya kufungwa bao la kwanza na
kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani hawawezi kuelezea
ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na unatakiwa kuheshimu hilo.
Tunatakiwa kujiunza jinsi ya
kukabiliana nalo. Ujumbe wangu kwa watu wa Brazil ni huu. Tafadhali watusamehe
kwa kiwango hiki. Ninaomba radhi kwasababu hatujaweza kufika fainali-na
tutajitahidi kushinda mechi ya nafasi ya tatu. Bado tuna sababu ya kucheza.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HAYA NDIO MANENO ALIYOTAMKA LUIZ FELIPE SCOLARI BAADA YA KUFUNGWA 7-1 NA UJERUMANI”
Post a Comment