Wednesday, July 9, 2014

MADEREVA BODABODA WALIA NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.



Kamati maalum ya madereva Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, wamemtaka mkuu wa mkoa Saidi Meck Sadiki  kusitisha agizo la vyombo hivyo kutoingia katikati ya jiji (Central Business District CBD).

Akizungumza  jana  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katibu wa kamati hiyo Daudi Laurian, alisema kuwa mkuu wa mkoa alitoa agizo hilo bila kuwashirikisha kwa kuwapa taarifa  viongozi wa madereva hao.

Laurian aliongezea kuwa, chakusangaza Mkuu wa Mkoa huyo hatoi maelekezo yenye ufasaha juu ya mipaka ya katikati ya jiji na wapi wanatakiwa kuweka maegesho.

“Kinachotushangaza sisi ni Sababu zinazotolewa ni kwamba bodaboda zinasababisha ongezeko la ujambazi, kama ni hivyo kwanini wasiweke utaratibu maalm wa pikipiki binasfi kwa Maana boda boda zote zilizopo zimesajiriwa na Sumatra pia zinatumia namba za usajiri zenye rangi nyeupe pia maeneo yote yanarangi maalumu zinazo tambulisha” alisema Laurian.

Pia alibainisha kuwa, baada ya tamko hilo kutolewa kumekuwa na udanganyifu kwani kila taasisi za usalama, watu binafsi na wahuni kujifanya ni wateule wa serikali ya mkoa kutekeleza agizo, hivyo huwakamata madereva hao na kuwachukulia fedha au kuwasingizia kesi ya kupaki sehemu isiyo sahihi.

Alisema, madereva waliokamatwa hutozwa pesa nyingi kuanzia shilingi 50,000/=, 100,000/=, 250,000/= hadi 450,000/= kiasi kinachozidi uwezo wa vipato vyao na kukinzana na kanuni za Sumatra.

“kamati inatamika kwamba madereva wote walio kamatwa waachiwe, pia wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam kututetea wanabodaboda haina maana kwamba wanamasilahi na wenye pikipiki ila ni wajibu wa viongozi kutetea wananchi wao hasa wakiwa wanaonewa”alisema Laurian.

Laurian aliongezea kuwa, endapo mkuu wa mkoa asipotekeleza hayo, kamati imeadhimia kufanya maandamano ya amani kwa madereva bodaboda wote ili kuweza kukemea unyanyasaji huo sambamba na kuipeleka serikali mahakamani.

0 Responses to “MADEREVA BODABODA WALIA NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.”

Post a Comment

More to Read