Wednesday, July 9, 2014
09 Jul 2014 WANAFUNZI WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA KWA KUKOSA NAFASI KIDATO CHA TANO MKOANI MBEYA.
Do you like this story?
WAHITIMU 39 wa kidato cha nne mwaka
jana katika Shule ya Sekondari Karobe jijini hapa wakiwa na wazazi wao, jana
waliandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kujua hatma yao baada Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa kuwapangia nafasi za kujiunga kidato cha
tano licha ya kufanya vizuri katika mitihani yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,
wanafunzi hao pamoja na wazazi wao, walisema kuwa waliamua kufika ofisi za Mkuu
wa Mkoa ili kujua hatima yake, baada ya kuona hawapewi majibu ya kuridhisha
kutoka kwa viongozi wa chini yake.
Walisema tangu wizara itangaze majina
kwa ajili ya kujiunga kidato cha tano wiki mbili zilizopita, wameshangazwa
kuona wanafunzi kutoka shule hiyo hawajapangiwa kwa ajili ya kuendelea na
masomo katika ngazi hiyo, licha ya kuwa na ufaulu mzuri.
Wanafunzi hao ambao wamepata alama za
daraja la kwanza hadi tatu, hawajui hatima yao kutokana na wizara husika
kushindwa kuwapangia shule kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
Nao wazazi ambao waliambatana na watoto
wao hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (CHADEMA) kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala
hilo, walisema kuwa tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina
ya wanafunzi waliofaulu kwa ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa,
hakuna majina ya watoto wao.
Mmoja wa wazazi hao, Lawrance Shimo,
alisema baada ya kufuatilia kwa kina ikiwemo kuuliza uongozi wa shule,
walibaini kuwa katika shule hiyo hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa
shule kwa ajili ya kuendelea na kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa
alama mzuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ 09 Jul 2014 WANAFUNZI WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA KWA KUKOSA NAFASI KIDATO CHA TANO MKOANI MBEYA.”
Post a Comment