Sunday, July 6, 2014
MECHI YA KIRAFIKI KATI YA MBEYA CITY VS PRISON WAONYESHANA UBABE.
Do you like this story?
Utovu wa
nidhamu, vurugu na rabsha za hapa na pale zilizosababisha Polisi wa kutuliza
ghasia kuingia katikati ya Uwanja ni miongoni mwa matukio yaliyobeba hisia za
wapenzi wa soka Jijini Mbeya ambao walitarajia kuona burudani ya kandanda kati
ya timu zenye mashabiki wengi Mbeya City na Prison za Jijini hapa.
Mchezo huo
umezikutanisha timu hizo ikiwa ni takribani miezi mitatu tangu kumalizika kwa ligi hiyo mwezi
Aprili mwaka huu huku Prison ikikumbuka majeraha ya kufungwa na Mbeya City bao 1-0
katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Wakicheza
kwa kujiamini na kutarajia kushinda mechi hiyo
timu ya Mbeya City walianza
kuonesha utovu wa nidhamu pale mchezaji wa timu hiyo Richard Peter
alipofanikiwa kutingisha nyavu za Prison katika dakika ya 25 ilhali mshika
kibendera wa kulia mirambo Shikungu akiwa amenyoosha kibendera kuashiria kuwa
mchezaji huyo alikuwa ameotea.
Hali hiyo
ilianzisha lawama dhidi ya mshika kibendera huyo na kusababisha Mbeya kutoelewana vyema ilhali wenzao wa Prison wakijitahidi kutumia
fursa hiyo kuonesha kiwango kizuri cha kandanda.
Kwa
takribani dakika 14 mchezo huo ulikuwa ni wa kuviziana kati ya Mbeya City na
Prison ambapo kunako dakika ya 44 ya mchezo Winga wa kulia wa MBEYA City Deus
Kaseke aliambaa ambaa na mpira kuelekea katika lango la Prison.
Kaseke
alitoa pasi iliyomkuta Paul Nonga ambaye alipiga shuti lililombabatiza kipa wa
Prison Mohamed Yusuf ambaye bila tahadhari aliondosha hatari kwa miguu na
kumbabatiza mlinzi wa timu yake Lugano Mwangama na kujifunga goli, dakika ya
44.
Hadi
mapumziko Mbeya City walitoka kifua mbele wakiongoza goli 1.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo Prison walizalimika
kucheza nusu baada ya mchezaji wao Jeremiah Juma kuzawadiwa kadi mbili za njano
kwa mchezo mbaya na kulazimika kutoka nje ya uwanja.
Awali
Prison walipata penati iliyolalamikiwa na wachezaji wa Mbeya City ambapo
mchezaji wao Deogratius Julius aliunawa mpira eneo la adhabu na kusababisha
wachezaji wa timu hiyo kumzonga mshika kibendera lakini hata hivyo penati hiyo
iliyopigwa na Ibrahimu Mamba ilipaa juu ya mwamba.
Zikiwa
zimesalia dakika chache kabla ya mechi hiyo kumalizika huku wachezaji wa Mbeya
City wakiamini kuwa wameshinda mechi hiyo, wachezaji wa Prison walilisakama
lango la Mbeya City kama nyuki na kusababisha goli lililofungwa kwa kichwa na
Frank William.
Kipenga
cha kumaliza mpira huo kilichopulizwa na mwamuzi wa kati Kayombo kilisababisha
kundi la wachezaji wa timu hiyo kuvamia uwanja na kumzonga mshika kibendera
Shikungu ambapo waamuzi wengine waliingilia kati kuzuia tafrani hiyo.
Hali hiyo
ilisababisha askari polisi kuingilia kati na kulazimika kuwatoa nje ya uwanja
waamuzi wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MECHI YA KIRAFIKI KATI YA MBEYA CITY VS PRISON WAONYESHANA UBABE.”
Post a Comment