Saturday, July 5, 2014
RAIS KIKWETE ATAKA UBORA ZAIDI WA BIDHAA ZA TANZANIA.
Do you like this story?
Rais Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara nchini
kuongeza juhudi za kuongeza ubora zaidi wa bidhaa zao ili ziweze kushindana
na zile za nje ya nchi.
Aidha Rais Kikwete amewapongeza washiriki wa maonesho ya 38 ya Biashara
ya Kimataifa kwa kuongeza ubora wa bidhaa ambao kila mwaka kumekuwa na
tofauti.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete wakati akitembelea
leo maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye
viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
“ Maonesho ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kwani kumekuwepo kwa
ongezeko la bidhaa, bidhaa zimefungwa vizuri tukiendelea hivi tunaweza
kushindana na bidhaa za kimataifa. Pendekezo langu mimi ni kuendelea
kufanya ziwe vizuri zaidi,” alisema Rais Kikwete.
Akitembelea banda la Jeshi la M,agereza, Rais Kikwete ambapo
alijionea uzalishaji wa bidhaa za kilimo, alilitaka jeshil hilo kutoa
elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora cha kisasa.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete alitembelea mabanda mbalimbali
likiwemo la Wakala wa Mafunzo nje ya nchi. Benki Kuu ya Tanzania, Bidhaa za
Tanzaniana mengineyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS KIKWETE ATAKA UBORA ZAIDI WA BIDHAA ZA TANZANIA.”
Post a Comment