Friday, July 4, 2014

TAKWIMU MBALIMBALI ZA KOMBE LA DUNIA KABLA YA MECHI ZA ROBO FAINALI.



Hatua ya robo fainali ya kombe la dunia inaendelea leo. Saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki, Ufaransa watachuana na Ujerumani.

Saa 5:00 usiku, wenyeji Brazil watakuwa kibaruani dhidi ya Colombia.
Kfikia sasa hizi ndio takwimu muhimu za kombe la dunia mwaka 2014, nchini Brazil.
Kufikia sasa mpaka michezo 56 kati ya 64 imekwishachezwa,
Takwimu muhimu mpaka sasa,
Mfungaji bora anayeongoza akiwa ni James Rodrguez wa Colombia mwenye mabao matano, huku Neymar, Lionel Messi na Thomas Muller wa Ujerumani wakifuatia wakiwa na mabao manne kila mmoja.

Jumla ya mabao 154 yamefungwa mpaka sasa, ikiwa ni wastani wa mabao matatu kwa kila mechi.
Mechi iliyoshuhudia mabao mengi zaidi yakifungwa ikiwa ni kati ya Uswiss na Ufaransa, ambapo jumla ya mabao saba yaliingia wavuni.

Uholanzi ndo timu iliyofunga mabao mengi zaidi mpaka kwenye michuano hii ikiwa na jumla ya mabao 12, mabao 11 yakifungwa kwa kupeana pasi huku bao moja likiwa ni kwa mpira uliokufa.

Ubelgji ndo timu iliyofanya mashambulio mengi sana langoni mwa timu pinzani, ikiwa imefanya mashambulizi 81 kwa timu zote ilizokutana nazo, huku Algeria ikiwa ndo timu iliyokaba sana na kuzuia mashambulizi mengi.
Ujerumani, Ni mabingwa wa kupiga pasi nyingi zaidi ambapo hadi sasa wamekishapiga pasi 2560. Ila Javier Macherano wa Argentina ndiye kinara wa kupiga pasi nyingi zaidi kwa wachezaji, akipiga jumla ya pasi 364.

Michael Bradely wa Marekani, ni Usain Bolt wa michuano hii akiwa ndiye mchezaji aliyekimbia sana uwanjani, akikimbia kwa jumla ya mile elfu 54, 709 sawa na kilometa elfu 88 na 45.

Kwa upande wa Makipa, Kelya Navas mlinda mlango wa Costa Rica ndiye kipa aliyeokoa michomo mingi zaidi kwenye michuano ya mwaka huu, ambapo amekwisha okoa michomo 14 iliyoelekea langoni huku akiruhusu kufungwa mabao mawili pekee.

Lakini mlinda mlango wa Nigeria, Austine Edje naye amejiandikia rekodi mpya ya kuwa mchezaji aliyeitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kwenye fainali tatu za michuano ya kombe la dunia lakini hajacheza hata mechi moja.

Rafael Marquez wa Mexico amekuwa nahodha aliyecheza fainali nne za michuano ya kombe la dunia, akianza toka mwaka 2002 nchini Japan hadi sasa Brazil ambapo timu yake ilitolewa na Uholanzi katika hatua ya kumi na sita bora.
Akiwa na umri wa miaka 43 Faryd Mondragon, mlinda mlango wa Colombia amevunja rekodi ya mkongwe wa Cameroon, Rogger Millar kwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kucheza mechi za kombe la dunia.
Naye Kinda wa Marekani anayekipiga kwenye klabu ya Bayern Munich, Julien Green amekuwa mchezaji wa saba kijana kufunga bao akiwa na umri mdogo kwenye michuano ya kombe la dunia, akiwa kwenye kundi moja na Lionel Messi wa Ajentina na Divock Origi wa Ubelgji.
Na
Kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya mwaka huu, vinara wa makundi wamefuzu kwa hatua ya robo fainali, wakishindwa kufungwa na timu zilizoshika nafasi ya pili kwenye makundi.

0 Responses to “TAKWIMU MBALIMBALI ZA KOMBE LA DUNIA KABLA YA MECHI ZA ROBO FAINALI.”

Post a Comment

More to Read