Friday, July 4, 2014
MUGABE AWAFUKUZA WAKULIMA WAZUNGU.
Do you like this story?
Rais
wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu waliosalia nchini humo
kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.
"hatuwataki
wakulima wazungu, kumiliki mashamba yetu, lazima waondoke,'' Mugabe aliwaambia
wafuasi wake katika mkutano wa hadhara.
Chama
cha wakulima wazungu, kimesema kuwa matamshi ya Mugabe yanasikitisha sana na
kwamba taharuki ya kibaguzi imeanza kutanda.
Wakosoaji
wa Rais Mugabe, wanasema kuwa sera yake kutaka kumiliki mashamba yote
yanayomilikiwa na wazungu, ndio ilisababisha kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo
kati ya mwaka 200-2009
Rais
Mugabe mwenye umri wa miaka 90, ametawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kujipatia
uhuru mwaka 1980.
Alichaguliwa
tena mwaka jana kwa asilimia 61 ya kura, na kumshinda mpinzani wake wa jadi
Morgan Tsvangirai.
Chama
cha Mugabe pia kilishinda viti vingi vya bunge na kupata 160 kati ya viti 210.
Mdadisi
wa kisiasa nchini humo Stanley Kwenda anasema kuwa matamshi ya Mugabe,
yanashangaza sana kwani serikali ilimaliza mageuzi ya sera ya umiliki wa
mashamba miaka miwili iliyopita.
Inaonekana
kwamba Mugabe anataka kuhujumu hali mbaya ua kiuchumi nchini humo kwa
kuzungumzia maswala mengine ambayo hayana umuhimu kwa sasa.
Wananchi
wa Zimbabwe wanakumbwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na kufungwa kwa
makampuni .
"usiwe
mkarimu sana kwa wakulima wazungu. Mashamba ni yako sio yao,'' alisema Mugabe
alipotembelea mkoa wa Mashonaland , Magharibi mwa nchi.
Mtamshi
ya Rais Mugabe, yalisababisha wasiwasi miongoni mwa wakulima wazungu. Hii ni
kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa wakulima wazungu Hendricks Olivier.
Ni
wakulima 100 hadi 150 wazungu waliosalia nchini Zimbabwe, alisema Hendricks.
Maelfu
ya wakulima walilazimika kuyaacha mashamba yao na kurejea walikotoka baada ya
serikali kufanya mageuzi ya sera ya umiliki wa ardhi miaka 15 iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MUGABE AWAFUKUZA WAKULIMA WAZUNGU.”
Post a Comment